Posts
KAMATI YAUNDWA UJENZI WA JENGO LA YANGA
- Get link
- X
- Other Apps
Ndugu Ridhiwani Kikwete, mwenyekiti wa kamati hiyo ya ujenzi wa majengo ya Yanga lililopo mtaa wa Mafia na Nyamwezi ameunda kamati ya wajumbe tisa(9) watakaosimamia ujenzi wa majengo hayo huko Zanzibar. Huku wajumbe wengine ni jaji mstaafu John Mkwawa, Naibu waziri wa wizara ya Miundombinu ya serikali ya mapinduzi Zanzibar,Allan Magoma,Charles Palapala,Izack Chanje na wakili Mavalle Msemo.
BAADHI ZA PICHA KATIKA TUKIO LA GHOROFA LILILOPOROMOKA ASUBUHI HII YA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.
- Get link
- X
- Other Apps
Kamanda wa Kanda maalum ya Kipolisi mkoa wa Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova kulia akizungumza jambo na Mbunge wa kuteuliwa Mh. James Mbatia ambaye ameungana na wananchi wengine katika tukio hilo. Uokoaji ukiendelea katika eneo la tukio. Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick akiwa katika eneo la tukio kusimamia zoezi la uokoaji. Ulinzi ukiwa umeimarishwa katika eneo la tukio Kibao hiki kinaonyesha kampuni ambazo zilikuwa zikijenga jengo hilo. Kijiko kikiendelea kuondoa kifusi katika eneo la tukio Wananchi wakishiriki katika zoezi la uokoaji kwa kuondoa taka na vifusi katika eneo hilo.
Mbunge wa CUF, Jimbo la Chambani Pemba Salim Hemed Khamis Afariki Dunia,Kuagwa leo, Asubuhi Viwanja Vya Karimjee Jijini Dar es Salaam Kuzikwa Pemba
- Get link
- X
- Other Apps
Mbunge wa CUF, Jimbo la Chambani Pemba kisiwani Zanzibar, Marehemu, Salim Hemed Baadhi ya Maofisa wa Ofisi Ndogo ya Bunge,wakimsaidia kwa kumbeba Mbunge wa Chambani,Bwa.Salim Hemed Khamis,mara baada ya kuanguka ghafla hapo juzi jijini Dar akiwa katika vikao vya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu ya haraka. -- MAZISHI ya aliyekuwa Mbunge wa CUF, Jimbo la Chambani Pemba kisiwani Zanzibar, Marehemu, Salim Hemed Khamis,yanataraji kufanyika leo mchana mjini Pemba. Taarifa za awali kutoka Chama cha Wananchi CUF, zinasema kuwa Mwili wa Marehemu, Khamis utaagwa leo asubuhi kuanzia majira ya saa 2:30-4:00 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam ambapo Viongozi mbalimbali wa kitaifa na Kimataifa pamoja na wananchi na Wanachama wa CUF watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu. Taarifa hiyo ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julis ...