Mbunge wa CUF, Jimbo la Chambani Pemba Salim Hemed Khamis Afariki Dunia,Kuagwa leo, Asubuhi Viwanja Vya Karimjee Jijini Dar es Salaam Kuzikwa Pemba


 Mbunge wa CUF, Jimbo la Chambani Pemba kisiwani Zanzibar, Marehemu,  Salim Hemed 


 Baadhi ya Maofisa wa Ofisi Ndogo ya Bunge,wakimsaidia kwa kumbeba Mbunge wa Chambani,Bwa.Salim Hemed Khamis,mara baada ya kuanguka ghafla hapo juzi jijini Dar akiwa katika vikao vya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu ya haraka.
--
MAZISHI ya aliyekuwa Mbunge wa CUF, Jimbo la Chambani Pemba kisiwani Zanzibar, Marehemu,  Salim Hemed Khamis,yanataraji kufanyika leo mchana mjini Pemba.
Taarifa za awali kutoka Chama cha Wananchi CUF, zinasema kuwa Mwili wa Marehemu, Khamis utaagwa leo asubuhi kuanzia majira ya saa 2:30-4:00  katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam ambapo Viongozi mbalimbali wa kitaifa na Kimataifa pamoja na wananchi na Wanachama wa CUF watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu.

Taarifa hiyo ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julis Mtatiro inasema kuwa Msafara utaondoka Karimjee saa 4:00 kuelekea uwaja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo Msafara wa Ndege 2 utaondoka kwenda Pemba.
Saa saba mchana mazishi yatafanyika huko Pemba na maazishi hayo yataongozwa na Viongozi wa serikali, Wabunge na CUF.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA