UJUMBE WA BODI YA KIMATAIFA YA PLAN INTERNATIONAL WATEMBELEA MIRADI YA SHIRIKA HILO IKIWEMO KITUO CHA WATOTO CHA MLEGELE-KISARAWE.


Wakazi wa Wilaya ya Kisarawe wakicheza ngoma ya kiutamaduni pamoja na mmoja wa wajumbe wa bodi ya Plan International waliotembelea moja ya miradi inayofadhiliwa na shirika hilo wilayani humo.

Mlezi wa Kituo cha Mlegele Wilayani Kisarawe na Mwenyekiti wa Majengo yote ya Kulelea watoto hao Bw. Shabani Daruweshi akisoma risala kwa ujumbe wa Bodi ya Plan International (haupo pichani) ambapo amesema Shirika la Plan International limeshirikiana kikamilifu na Wanajamii, Serikali na Mashirika mengine katika kufadhili taratibu zote za kuwajengea uwezo wa kitaalam wadau mbalimbali, akitolea mfano kuijengea uwezo wa kitaalam timu ya Wilaya ya wataalam wa malezi na makuzi ya mtoto katika wilaya ya Kisarawe.
Amesema pamoja na mafanikio waliyoyapata bado wankabiliana na changamoto kadhaa ikiwemo Miundo Mbinu ya kituo kutokuwa rafiki wa watoto ikiwa ni pamoja na majengo ya kudumu, uhaba wa maji safi na salama, upungufu wa vyumba vinne vya madarasa kwa ajili ya shule ya msingi, nyumba ya walimu, ofisi, kituo cha afya ili kupunguza umbali wakupata elimu ya msingi kwa wakazi wa Mlegele.

Mlezi wa Kituo cha Mlegele Wilayani Kisarawe na Mwenyekiti wa Majengo yote ya Kulelea watoto hao Bw. Shabani Daruweshi akikabidhi risala kwa ujumbe wa bodi ya kimataifa ya Plan International ambao umesheheni changamoto kadhaa zinazohitaji kutatuliwa.

Ujumbe wa Bodi ya Kimataifa ya Plan International uliotembelea Kituo cha watoto cha Mlegele kilichopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

Baadhi ya Wakazi wa Kisarawe mkoani Pwani wakisiliza yaliyokuwa yakizungumzwa na Ujumbe wa Kimataifa kutoka Plan International.

Mkufunzi wa Wauguzi Bi. Maseif Mchachura akitoa chanjo kwa mmoja wa watoto eneo la Mlegele Wilayani Kisarawe wakati Ujumbe wa bodi ya Plan International ulipotembelea eneo hilo na kukagua miradi inayofadhiliwa na shirika hilo.

Gari la kutoa huduma za mbalimbali za tiba lililotolewa na Daichi Sankyo kupitia shirika la Plan International linalotoa huduma kwa jamii ya Wakazi wa Mlegele wanaoishi wilayani Kisarawe mkoani Pwani ambapo huzunguka kuwasaidia watoto wachanga wanaozaliwa hadi wamama wajawazito na wengineo.
Mfanyakazi wa Plan International kutoka nchini Kenya Grace Ndungu akichukua maelezo kutoka kwa Mkufunzi wa Wauguzi Bi. Maseif Mchachura annayetoa huduma katika Mobile Clinic iliyopo Wilayani Kisarawe kwa niaba ya Plan International.

Mkufunzi wa Wauguzi Bi. Maseif Mchachura wa Mlegele Wilayani Kisarawe akionyesha ujumbe wa Bodi ya Plan International dawa wanazotumia kusaidia kinamama pamoja na watoto wanaogua hata watu wazima wanaopata Malaria na magonjwa mengineo.

Ujumbe wa Bodi ya Plan International ukizungumza na watoto wa shule ya awali ya kituo cha Watoto cha Mlegele ambacho kimedhaminiwa na shirika hilo kuhakikisha watoto wenye umri wa kuanza shule wanaweza kupata elimu hiyo.
Mmoja wa watoto wa shule ya Awali ya Mlegele akipata kikombe cha uji.

Mmoja wa wafanyakazi wa Plan International Tanzania akionyesha jiko linalotumiwa kupika uji kwa ajili ya watoto wa shule hiyo ya awali kwa ujumbe wa bodi ya Plan International iliyotembelea kituoni hapo kukagua miradi inayofadhiliwa na Plan International.

Kichanja cha kuanikia vyombo vinavyotumiwa na watoto wa kituo cha Mlegele kunywea uji.
Baadhi ya watoto wa shule ya msingi katika kituo cha watoto cha Mlegele wakati wa ziara ya ujumbe wa bodi ya Plan International ulifika Kisarawe kukagua miradi ya Shirika hilo.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA