SPIKA WA BUNGE AWASILI CANADA MJINI QUEBEC

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili katika uwanja wa ndege mjini Quebec, Canada tayari kwa kuhudhuria mkutano wa 127 wa chama cha Mabunge Duniani (IPU) unaotarajia kufunguliwa rasmi kesho tarehe 21 Oktoba, 2012 na kumalizika 26 Oktoba . Makinda ameongoja ujumbe wa wabunge wanne kutoka Tanzania, ambapo zaidi ya maspika wa nchi 150 duniani wakiongoza ujumbe wa wabunge kutoka Nchi zao watashiriki mkutano huo.
Spika wa  Bunge Mhe. Anne Makinda akiteta jambo kuhusu  maandalizi ya awali ya mkutano na afisa kutoka Bunge la Canada mara alipopokelewa baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege mjini Canada kuhudhuria mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani. Kulia ni Mhe. David Kafulila na Mhe. Hamad Rashid waliongozana na Mhe. Spika katika Mkutano huo nchini Canada
Mhe. Spika  Anne makinda na ujumbe wake wakionyesha nyaraka muhimu za kusafiria kwa ofisa wa uwanja wa ndege mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege  baada ya kuwasili mjini Quebec nchini Canada kuhudhuria Mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU)

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA