MWILI WA KARDINALI LAUREAN RUGAMBWA KUZIKWA UPYA OKTOBA 6, BUKOBA
Marehemu Kardinal Laurean Rugambwa enzi ya uhai wake.
Kanisa kuu katoliki jimbo la Bukoba ambalo masalia ya marehemu kardinali Rugambwa yatazikwa ndani yake.
*************
MWILI WA KARDINALI LAUREAN RUGAMBWA KUZIKWA UPYA OKTOBA 6, BUKOBA
Kanisa
katoliki nchini dayosisi ya Bukoba mkoani Kagera, wanajiandaa kuzika
upya masalia ya mwili wa aliyekuwa askofu wa dayosisi hiyo Kardinali
Laurean Rugambwa, aliyefariki mnamo mwaka 1997 katika kanisa kuu la
Bukoba. Maziko ya Kadinali Rugambwa yamepangwa kufanyika siku ya oktoba 6
mwaka huu.
Mwili
wa askofu huyo wa kwanza nchini na Kardinali wa kwanza mweusi barani
Afrika umezikwa katika kanisa la kwanza mkoani Kagera lililopo Kashozi
kutokana na kwamba kanisa kuu la Bukoba ambalo marehemu aliagiza
kuzikiwa ndani yake lilikuwa katika matengenezo makubwa.
Akizungumza
katika kipindi cha Baragumu Channel ten na baadaye kwenye mkutano na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Askofu msaidizi wa Jimbo la
Bukoba Askofu Methodius Kilaini , amesema wanataka kumzika kardinali
Rugambwa kwa heshima tena katika kanisa alilopenda kuzikiwa kutokana na
kukamilika kwake, lakini kabla ya kuzikwa humo kutatanguliwa na ibada
mbalimbali ikiwa sehemu alikozaliwa, alikobatizwa, sherehe
zitakazoambatana na kusherehekea miaka 100 ya kuzaliwa kwa kardinali
Rugambwa tarehe 7 mwezi Octoba.
"tuna
alika watu wengi kuhudhuria kwenye tukio hili..., na pia tunakaribisha
michango itakayowezesha kuwa na kitu cha kumkumbuka marehemu kwa
mchango wake,alisema askofu Kilaini.
Naye
mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya kufanikisha tukio hilo ,
James Rugemalira, alimwelezea Kardinali Rugambwa kama mtu aliyetoa
mchango mkubwa kwenye jamii ya watanzania, kuanzia kwenye nyanja za
elimu, afya na kiroho.
Marehemu
Kardinali Rugambwa ana mambo mengi ya kukumbukwa na jamii ya
watanzania hususani watu wa mkoa wa Kagera hasa kwa juhudi zake za
kupeleka elimu mkoani humo kwa kuagiza ujengwaji wa shule za msingi na
sekondari ikiwemo shule ya kwanza ya wasichana ya Rugambwa ambayo
ujenzi wake ulikuwa ni mafanikio ya marehemu huyo kuomba msaada wa
ujenzi wa shule hiyo alipohutubia bunge la Ujerumani akiwa mwafrika wa
kwanza.
Licha
ya mambo hayo yote kanisa hilo pia liko mbioni kuanzisha mfuko rasmi
wa kumuenzi kardinali huyo mfuko utakaojulikana kwa jina la Kardinali
Rugambwa ambao utakuwa maalumu kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali
za kijamii.
Padre
Laurean Rugambwa aliwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 10
Februari,1952. Alizaliwa julai 22 1912 na kufariki miaka 15 iliyopita.