Warembo wanaotarajia kupanda jukwaani kuwania Taji la Miss Vyuo Vikuu 2012, siku ya Ijumaa wiki hii katika Ukumbi wa Maisha Club, wakipozi kwa picha ya pamoja nje ya Ukumbi wa Bunge, wakati warembo hao walipofika kutembelea na kujifunza shughuli za Bunge mjini Dodoma Leo, Julai 03, 2012
CATHERINE MASUMBIGANA AWA REDD'S MISS CHANG'OMBE
Redds Miss Chang’ombe 2012, Catherine Masumbigana 21, (katikati) akipunga mkono mara baada ya kusimikwa rasmi kuwa mshindi wa taji hilo. Kulia ni mmshindi wa pili, Jesca Haule (18) na Mshindi wa tatu Zulfa Bundala. Masumbigana aliwashinda warembo wengine 13 katika shindano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Quality Center jijini Dar es Salaam Juni 10, 2012. Tano bora ya Miss Chang’ombe 2012 ambao wote wamepata tiketi ya kushiriki shindano la Miss Temeke 2012 wakiwa katika picha ya pamoja. Kutoka Kushoto ni Zulfa Bundala (21), Jesca Haule (18), Catherine Masumbigana (21), Miriam Nkisigwa (20) na Flora Kazungu. Warembo wakicheza show maalum ya ufunguzi Vazi la ufukwenu, Kutoka kulia ni Restituta Faustiney, Wensley Mabula na Clara Diu. Warembo Flora Mayasa (kulia) Catherine Masumbigana (katikati) na Elizabeth Mushi wakiwinda point na vazi la ufukweni. Mkali wa Bongo Fleva Nassib Abdul 'Diamond' na vija...

