ILALA IMEJIPANGA VYEMA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO


Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza katika mkutano huo
Wajumbe wa mkutano huo wakiwa katika mkutano


 

Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mhe. Jerry Silaa katika mkutano wa kujenga uelewa kwa viongozi kuhusu program  ya kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto.
Akifungua mkutano huo Mhe. Silaa alisema kuwa Manispaa ya Ilala inashiriki kikamilifu katika  utekelezaji wa malengo ya milenia ya kupunguza vifo vya  akina mama na watoto.
Alieleza kuwa katika Manispaa ya Ilala kuna vituo mbalimbali vilivyopo katika Hospitali na zahanati kwa ajili ya kupima virusi vya UKIMWI na kuwapatia wathirika wa UKIMWI dawa za kurefusha maisha. Alisema kitu muhimu tunachoijikita nacho hivi sasa ni kupunguza maambukizi ya virusi ya UKIMWI kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto.
Alisema kuwa Manispaa ya Ilala ina watalaam wa  kutosha wenye uelewa mkubwa wa afya ya Mama na mtoto. ’Ndoto yetu ni kuwa na kizazi kisicho kuwa na maambukizi ya UKIMWI “ alisema Mhe. Silaa. Alibainisha kuwa nia ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ni kuwa na watoto watakaozaliwa bila ya maambukizi ya UKIMWI kufikia mwaka 2015.
Programu hiyo ya kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto inafadhiliwa na Taasisi ya Management Development to Health (MDH) ambayo imejikita kwenye mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI.
Akifafanua kazi zianazofanywa na MDH Dr David Sando ambaye ni Mkurugenzi wa mikakaati ya mawasiliano wa Taasisi hiyo, alisema kuwa MDH kama mdau  Serikali katika afya imejikita katika kutengeneza miundo mbinu ya afya , kujenga Kliniki za kupima maambukizi ya virusi vya UKIMWI pamoja na ukarabati wa Kliniki hizo.
Alisema kuwa MDH katika Manispaa ya Ilala wamekuwa wakihakikisha hakuna upungufu wa rasilimali watu. Aidha, alisema wamekwisha endesha mafunzo endelevu kwa wataalam hao ili waweze kutoa huduma bora.

Alitaja huduma nyingine wanayotoa ni ya kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto kwa kuhakikisha mama anazaa vizuri na mtoto anazaliwa salama bila ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Taasisi  ya MDH imeanza kazi zake nchni Tanzania tangu mwaka 2000 kwa hisani ya full shangwe blog.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA