Zaidi ya watu 50 wafariki dunia kwenye ajali ya boti nchini Malawi

 Habari kutoka Malawi zinasema kuwa zaidi ya watu 50 wamefariki dunia kwenye ajali ya boti iliyotokea katika ziwa Malawi. Maafisa wa polisi wa nchi hiyo wamesema kuwa boti hiyo ilikuwa na wahajiri haramu kutoka Somalia na Ethiopia ambao lengo lao lilikuwa ni kufika Malawi na kisha kuingia kinyemela Afrika Kusini. Baadhi ya duru zinaarifu kuwa Watanzania kadhaa pia ni miongoni mwa waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo. Imedaiwa kwamba boti hiyo ilizama siku ya Jumanne na miili kuanza kuelea siku iliyofuatia. Maafisa wa usalama wamesema kuwa tayari miili 47 imeopolewa na kuzikwa kwenye kaburi la pamoja. Ripoti ya hivi majuzi ya shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch imesema visa vya magendo ya binadamu barani Afrika vimezidi mno katika miezi minne ya kwanza ya mwaka huu wa 2012 ikilinganishwa na miezi minne ya kwanza ya mwaka uliopita.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA