WASHINDI WENGINE WANNE WASHINDA ZAWADI ZA SBL

Kampuni ya bia ya Serengeti imekuwa ikizunguka katika mikoa mbalimbali hapa nchini kukabidhi zawadi kwa washindi wa zawadi hizo katika promosheni inyoendelea’VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO NA SBL, inayoendeshwa na kampuni hiyo kwa kipindi cha wiki 7 sasa na kubakisha takribani wiki 9 ili kuisha kwa promosheni hiyo ya kipekee kabisa kutokea hapa nchini Tanzania  hakika watanzania wengi wananufaika na kupiga hatua mbele kimaisha.A

Asubuhi ya leo droo ya nne katika promosheni hiyo ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’ imechezeshwa katika ofisi za kampuni ya bia ya Serengeti SBL zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini na kuhudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH MOBILE, wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers.

Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia vinywaji vyake aina ya Serengeti premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni hiyo nchi nzima ambapo kwa mara nyingine wikim iliopita wadau,washiriki na watanzania wote walishuhudia washindi wa bajaj na pikipiki wakikabidhiwa zawadi zao huko mafinga na Iringa mjini mkoani Iringa.Mshindi wa mafinga aliwa bw. Fadhili Manzi aliyejishindia bajaj mpya, kutoka iringa mjini ni bw. Octavian Chagula ayeibuka na pikipiki mpya kabisa.

Akionge na wandishi wa habari wakati wa kuchezesha droo hiyo, meneja wa bia ya serengeti lager bw. Allan Chonjo amesema lengo hasa la promosheni hiyo ni kujaribu kusaidia jamii kwa njia ya bahati na nasibu ili kuwafikia watanzania wengi zaidi bila upendeleo.

“ Bado tunaendelea kuwahamasisha wateja wetu na watanzania wote wenye umri unaruhusu kushiriki katika promosheni hii waendelee kushiriki bila kukata tamaa kwani bado kuna zawadi nyingi sana hadi zifikie milioni 780.

Washindi wetu katika droo hii ya saba ni Salvatory Herald 52 kutoka Tanga na Leonard Mkumbwa kutoka Dar es Salaam ambao wote kwapamoja wamejishindia jenereta, na Jacob Mgendi 27 kutoka Mwanza ambaye amejinyakulia bajaj mpya huku Mbaraka Adam32 kutoka kiwalani jijini Dar es Salaam akiibuka na pikipiki mpya kabisa zawadi zote kutoka SBL ambapo kwa mara ya tatu mfululizo, washindi wa bajaj wamekuwa wakipatikana Mwanza na kufikisha idadi ya bajaj 3 kutoka SBL mkoani mwanza.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA