UVCCM YAFANYA KIKAO
Baraza
la Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa waendelea na vikao
ambavyo vinafanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Makao Makuu ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dodoma.
Vikao
hivyo ambavyo vilianza rasmi tarehe moja June 1, 2012. Vinaendelea leo
hii hapa Dodoma, ambapo hoja mbalimbali zimekuwa zikijadiliwa kwa
kina, ambapo vikao vilivyotangulia vimejadili juu ya hoja ya Katiba
Mpya na suala la Muungano wa Serikali ya Jamhuri ya Muun gano wa
Tanzania. Ambapo wajumbe walichangia hoja mbalimbali za msingi kwa
kuzingatia hali ya sasa ya siasa nchini na matukio sambamba na hoja
hiyo, kama vile mijadala ndani ya majukwaa mbalimbali juu ya muundo wa
Katiba ya sasa, mapungufu yake na mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya
na pia mijadala juu ya maboresho ya Muungano.
Pamoja na hayo, kikao kinachoendelea hivi leo,kitajadili juu ya mapendekezo ya jinsi ya kuimarisha na kuboresho Umoja huo wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).