UHABA WA MADAWATI MUSOMA

UHABA wa madawati katika shule za msingi na sekondari umeendelea kuumiza vichwa vya wapenda elimu pamoja na wazazi kwa ujumla nchini, ikiwemo Shule za Wilaya ya Musoma Vijijini.

Upungufu wa madawati katika shule za msingi umeendelea kudidimiza kiwango cha elimu nchini huku ukichangia kuongezeka kwa utoro kwa kusababisha wanafunzi wengine kukata tamaa ya kusoma na mazingira ya shule kwa ujumla ambayo si rafiki kwao.


Matokeo ya wanafunzi kukaa chini husababisha wanafunzi kuandika wakiwa wameinama na wengine hata kulala kifudi fudi na wengine kuchuchumaa na hivyo kushindwa kuandika vizuri na pia kuchoka mapema. Hali hii kupelekea matokeo mabaya nyakati za mitihani hasa ya kitaifa.


Wanafunzi wa Shule ya Msingi Etaro wakiwa darasani wakimfuatilia mwalimu. wanafunzi wengi katika shule hii wanakaa chini kutokana na uhaba wa madawati

Popular posts from this blog

CATHERINE MASUMBIGANA AWA REDD'S MISS CHANG'OMBE

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

HOTUBA YA MHESHIMIWA PEREIRA AME SILIMA (MB), MWENYEKITI WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI (T)