SWALA LA AFYA YA UZAZI LIPEWE KIPAUMBELE KWENYE MCHAKATO WA KATIBA MPYA
Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA Mwanasheria Tike Mwampipile akizungumza na washiriki wa semina ya mapendekezo ya kuwepo kwa sheria ya Afya ya Uzazi Salama katika
mchakato wa maoni ya kuandikwa kwa Katiba Mpya iliyomalizika jana
kwenye ukubi wa hoteli ya Blue Pear Ubungo Plaza jijini Dar es salaam.
NA MAGRETH KINABO- MAELEZO
JAMII iimeshauriwa kulipa kipaumbele suala ya mapendekezo ya kuwepo kwa sheria ya Afya ya Uzazi Salama katika
mchakato wa kuwepo kwa Katiba Mpya , ambayo itawezesha watumishi wa
afya ambao watasababisha vifo vya wakinamama wajawazito au watoto wachanga kwa sababu za uzembe.
Kauli hiyo iliyoilitolewa (jana) na Mkurugenzi wa Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA), Tike Mwampipile, wakati akifafanua ya mapendekezo hayo iliyoandaliwa na
chama hicho kwa waandishi wa habari kwenye semina ya siku mbili
iliyofanyika , Ubungo Plaza jijiini Dares Salaam.Semina ya mafunzo hayo ambayo iliyoanza jana (juzi) na kumalizika leo(jana)
“ Wito wangu katika jamii ni ni ina wajikubu mkubwa wa kujua haki zao
za msingi na kufahamu wapi pa kuzipata. Afya ya Uzazi Salama ni kitu
muhimu ambacho hakijangaliwa kwa umakini. Hivyo katika mchakato wa
Katiba Mpya suala hili liangaliwe kwa uzito kwa na upana wake kujali mama ambaye analemta mtoto hapa duniani ambaye anaweza kuwa na Rais au Waziri Mkuu wa kesho,” alisema Mwampipile.
Aliongeza kuwa kuwepo kwa sheria hiyo kutasaidia kupunguza idadi ya vifo vya wakinamama wajawazitio na watoto wachanga.
Kwa upande wake mtoa mada wa mapendekezo hayo, Bernadetha Mkandya ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya TAWLA na Wakili wa Kujitegemea alisema kuwa mwanamke ana haki ya kuishi na kulindwa ,hivyo sheria hiyo italuiwezesha taifa kupata watoto waliolelewa katika mazingira bora na afya njema. .
“ Tunataka tuwe na sheria ya iyatomlinda mwanamke wakati wa ujauzito na siku 42 baada ya kujifungua,” ikiwepo kupanga idadi ya watoto atakaoweza kuwalea na muda wa kupata mtoto mmoja baada ya mwingine alisema.
Akifafanua zaidi kuhusu sheria hiyo alisema itamwezesha
mamamjamzito kupata huduma za afya ya uzazi salama bora na ambazo
zitamwezesha kupata vifaa tiba vinavyotakiwa bila gharama yeyote.
Aidha Mkandya aliongeza katika sheria hiyo wamapendekeza kuwa umri wa
uti mzima uwe ni miaka 18 ili kuwezesha mtoto wa kike kuolewa katika
umri unaotakiwa hatua ambayo itasaidia kupunguza athari za afya ya uzazi
zinazotokana na umri mdogo. Alisisitiza kuwa ni muhimu
kwa makundi yote katika jamii kushiriki katika kutoa maoni ya mchakato
huo.
Mkandya aliongeza kuwa mapendekezo hayo hayo
yanaelekeza kuwepo kwa sheria ambayo itamwezesha mama mjamzito
kusitisha ujauzito pale itakapogundulika kuwa unasabbaisha athari za
kiafya kwa ruhusa ya daktari na ridhaa yake au endapo atakuwa amebakwa na kwa ridhaa yake kuwa hana uwezo wa kuendelea hudumia ujauzito huo na kumlea mtoto pale atakapojifungua.
Pia ridhaa hiyo inaweza kutolewa na ndugu zake endapo mama huyo ni mlemavu wa akili