THE SPECTRUM BAND


Mara ya Kwanza Kuwaona Spectrum Band Wakifanya kweli Jukwaani Sikuamini kama kazi 

nzuri inaweza kufanywa na wadada pasipo Mkono wa Mwanaume yeyote, na hii ikaanza kuondoa 

Mfumo dume wa mawazo uliokuwa ukitawala ufahamu wangu.

Blog ikatamani Kuwafahamu kwa Kiasi The Spectrum Band walio na Makazi yao ndani ya Jiji la 

Dar-es-Salaam.

Mazungumzo yangu na kundi hili la Muziki wa Injili katika Jiji la Dar-es-Salaam yalikuwa kama ifiatavyo.

Blogger: Nawasalimu kwa jina la Yesu.
TSB: Asante Papaa naona leo umetupata.
Blogger: Penye Nia Pana njia
TSB: Kwa Kweli
Blogger: Hongereni sana kwa kazi mnayoifanya ya kumtumikia Mungu kwa njia hii ya uimbaji wa nyimbo za Injili.
TSB: Asante Ubarikiwe na wewe Pia kwa kazi zako maana mmh.
Blogger: Kundi lenu linaitwa Spectrum nini maana yake?
TSB: Spectrum kwanza lina maana ya "Upinde Wa Mvua". Una rangi nyingi lakini ndo upinde wenyewe, through our differences we can accomplish something. Tunaamini ingawa tuko tofauti makabila tofauti lakini twaweza fanya kitu cha maana na kikubwa.
Blogger: Kundi hili la The Spetrum lilianza lini rasmi??
TSB: Kundi letu lilianza kazi rasmi tarehe 21 Mwezi August Mwaka 2009.
Blogger: Kundi hili la TSB linaundwa jumla na Wanamuziki Wangapi??
TSB: Kundi hili linaundwa na Jumla ya Akina dada Warembo Watano
Blogger: Kazi yenu kubwa hasa ni nini kama group.
TSB: Sisi tunafanya huduma ya Praise and Worship Makanisani, Mikutanoni, Kwenye Semina, Makongamano, Camps na kwingine kokote penye kuhitajika huduma hii.
Blogger: Dhu, naona mmekuja kivingine, nini matarajio yenu ya baadae kama group??
TSB: Tuna mpango wa kufungua Kampuni Tanzu hivi Karibuni itakayokuwa inafanya kazi mbalimbali, mojawapo ya maeneo tutakayo invest ni Salon za Kike na Za Kiume, Catering, Fashion and Designing na Events Managements.
Blogger: Kweli nyie wanawake wa kazi, changamoto kubwa ya akina dada ni kuendelea na maono mara baada ya kuolewa, mmejipangaje na hili kwa siku za usoni??
TSB: Kati ya watano ni mdada mmoja tu ambaye ameolewa, wengine bado wanamngoja Bwana, katika hili tumekuwa tukimwomba Mungu, lakini pia tunakusudia kuwaeleza hao wataokuwa waume zetu nini ambacho kipo ndani yetu ili wawe sababu ya kuchochea na sio kuua huduma.
Blogger: Kama group kuna mambo mnayapenda ni yepi??
TSB: Tunapenda kumtumikia Mungu, tunapenda kuwa na marafiki, tunapenda kucheza na Kuimba kwa Ujumla.
Blogger: Kuna mafanikio ambayo kama group mmefikia??
TSB: Ni kweli kabisa Mungu ametuwezesha tumekamilisha Albam yetu pamoja na ugumu tuliokuwa nao.
Blogger: Kama group nini kwazo kwenu na hampendi kuona nn kinatokea kwa kundi lenu?
TSN: Kama kundi hatupendi unafiki, hatupendi Majivuno na tunachukia dhambi.
Blogger: Niwatakie Utumishi Uliotukuka.
TSN: Amen.

Popular posts from this blog

CATHERINE MASUMBIGANA AWA REDD'S MISS CHANG'OMBE

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

HOTUBA YA MHESHIMIWA PEREIRA AME SILIMA (MB), MWENYEKITI WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI (T)