SINA MSUGUANO NA WAZIRI

WIZARA
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imekanusha taarifa kuwa
kunamsuguano kati ya Waziri na Katibu Mkuu katika Wizara hiyo.
Kauli
hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Seth Kamuhanda wakati
alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo .
Alisema
taarifa hizo zilizoandikwa na Jukwaa la wa Hariri Tanzania (TEF),
kwenye vyombo vya habari kuwa hazina ukweli wowote kwani viongozi hao
wamekuwa na ushirikiano mzuri kati kazi hivyo si rahisi kutokea
migongano kama ilivyodaiwa.
Kamuhanda
alisema nawaomba wanahabari mkitoka hapa muwafikishiye taarifa hizi
wananchi kuwa katika Wizara hiyo hakuna migongano na wahakikishia kuwa
haitatokea kwa kuwa hakuna tofauti yeyote kati yao.
"Unajua
hali kama hiyo ya mimi kugongana na waziri kwa kuwa kila mmoja wetu
amekuwa akifanya kazi yake kwa uadilifu mkubwa hivyo basi haitatokea
hata siku moja kutokea tofauti.
Akizungumzia
ni kwa nini walishindwa kufika siku ya kufungua na kufunga mkutano huo
alisema taarifa waliyopaswa kujibu na Baraza la Wahariri kutokana na
ukweli kwamba waliwafikishia taarifa ya kutofika.
Kamuhanda
alisema wakati walipopata mwaliko kipindi hicho Wizara ilikuwa katika
maandalizi kuhusu kamati za Bunge jambo ambalo liliwafanya washindwe
kuhuria kikao hicho ambapo walifikisha taarifa kwa Watendaji wa jukwaaa.
"Kwa kweli nilishangaa niliposoma hiyo taarifa kwa kuwa tulikwisha zungumza kuhusu kutohudhuria kwetu katika kikao hicho.