
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais Somalia Mheshimiwa Sheikh
Shariff Sheikh Ahmed leo Mei 4, 2012 kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Kilimanjaro, baada ya mgeni huyo kuhitimisha ziara yake ya siku
mbili nchini. Rais huyo wa Somalia alikuja nchini kwa mazungumzo na
Mheshimiwa Rais Kikwete ambapo alitoa shukurani zake kwa Tanzania
kutokana na misaada mbalimbali ya kibinadamu iliyopata na inayoendelea
kupata pamoja na kuisemea vyema Somalia katika medani za Kimataifa na
za Kikanda kila alipopata nafasi hiyo. PICHA NA IKULU