NAPE AFANYA MAMBO MJI WA SONGEA

Chama Cha Mapinduzi (CCM)
leo kimeiteka Songea, baada ya umati wa wananchi wa mji huo kuhudhuria
kwa wingi mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Majimaji.
Pichani, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, CCM, Itikadi na Uenezi
Nape Nnauye akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili kwenye Uwanja
huo. (Picha na Bashir Nkoromo)
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM ),Nape Nauye
amesema kuwa si sahii kwamba chama hicho kimepoteza mvuto na kukimbiwa
na vijana bali hiyo ni propaganda ya uongo na ni vita ya kisaikolojia
inayoendeshwa na vyama vya upinzani ambavyo alidai kuwa ni makundi ya
wapiga kelele ambayo hayapaswi kupewa madaraka ya kuongoza Nchi.
Alitoa
kauli hiyo jana mjini Songea mkoani Ruvuma wakati akiwa kwenye ziara
ya siku moja ya kukijenga chama hicho mkoani humo ambapo alipokelewa na
mamia ya wananchi na wapenzi wa chama hicho katika eneo la shule ya
tanga katika manispaa ya Songea alipoingia wakati akitokea mkoani
Iringa.
Awali
baada ya kusikiliza ujumbe toka kikundi cha ngoma cha ya lizombe cha
kiwanda cha kukaushia Tumbaku cha Sontop ambacho kimekufa na kilitoa
ujumbe uliomuomba kusimamia viongozi wa serikali mkoani humo
kuhakikisha kiwanda hicho kinafufuliwa kwa kuwa kilikuwa kikitoa ajira
kwa zaidi ya wananchi 2000 ya mkoa huo na kukuza uchumi wa Mkoa wa
Ruvuma.
Nape akijibu ujumbe huo alisema kuwa atahakikisha kiwanda hicho
kinafufuliwa kwa kuwa amekuja kukagua na kuona kasi ya maendeleo ya
miradi waliyoihaidi wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 na
wanatambuwa kuwa wamepewa dhamana kubwa ya kuhakikisha wananchi wanakuwa
na maisha bora .
“
Tutawashugulikia watendaji wabovu wa serikali kwa kuwa kwa utendaji
wao mmbovu wanasababisha chama chetu kichukiwe na wananchi kwa hiyo
kabla ya kuvuna mabua hatutaki kucheka na nyani “alisema Nauye.
Akizungumza
na wanachuo wa chuo kikuu cha mtakatifu Agustino tawi la Songea ambao
pia ni wapenzi wa CCM alisema kuwa takwimu zinaonyesha vijana bado
wanamapenzi na chama hicho ila wanakwazwa na vita ya kisaikolojia
inayoenezwa na vyama vya upinzani kwamba chama hicho kimepoteza mvuto
kwao.
Katika
kulitambua hilo alisema chama chake kimetenga utaratibu maalum ili
kuwajali na kwatambua vijana wake waliovyuoni kwa kutenga Mkoa maalum
wenye uongozi kamili ambao utajenga mtandao maalum utakao waunganisha .
Alisema utaratibu
huo pamoja na mambo mengine utashughulikia kero zinazowakabili
wananfunzi kwa kuwa kunautaratibu wa ovyo umejengeka wa bodi ya mikopo
kupeleka fedha za mikopo za wanafunzi baada ya kuandamana kuzidai fedha
hizo.
“Chama
chetu kinawajari sana vijana na ndio maana wanaonekana wako vizuri kwa
kuwa ukitaka kuona maendeleo ya Nchi angalia vijana wake na hivyo
katika utaratibu niliousema tutatengeneza kanuni ya kukaa mwaka mmoja
madarakani badala ya miaka mitano ili kuwapa nafasi zaidi vijana wetu
katika mikoa maalum tunayopanga kutenga kichama.”alisema.
Akitoa
dozi kwa vyama vya upinzani kama mwenyewe anavyodai alisema wanoota
kupata robo ya hadhi ya CCM wanaota ndoto za mchana na kwamba wameweka
mifumo mizuri kwenye chaguzi za chama ili mtu agombee kutokana na uwezo
wake kiuongozi na kutokana na uwezo wa fedha zake.
Alisema
utaratibu huo unakuja ili kufuta dhana iliyojengeka kwamba chama hicho
kiko kwaajiri ya watu wenye fedha na kwamba utaratibu wa chama hicho
kuwakumbatia watu wenye fedha ni kukiweka rehani.
Aidha
katika ziara yake hiyo ya siku moja ametembelea miradi mbalimbali ya
chama ,kuweka jiwe la msingi kwenye maduka ya biashara ya kupangisha ya
chama hicho yalijengwa eneo la Mshangano mjini hapa na kuzindua shina
la wakeleketwa la mshikamano ambalo amelichangia sh.300,000 na kuwataka
wafanyie shughuli za ujasilia mali.