MWILI WA ALIYEKUWA MHARIRI MKUU WA GAZETI LA JAMBO LEO UKIWASILI JIONI YA TAREHE 17 JUNE MWAKA HUU

Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concerpts Beny Kisaka na Juma Pito wakimfariji mdogo wake na marehemu Willy Edward mara baada ya kuwasili katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako mwili wa marehemu umehifadhiwa, Willy Edward alifariki usiku wa kuamkia leo mkoani Morogoro ambako alikuwa akihudhuria semina  ya Sensa kwa matatizo ya Moyo, Mwili wa marehemu Willy Edward utasafirishwa kwenda nyumbani kwao Mugumu Serengeti mkoani Mara kwa mazishi
Mwili wa marehemu Willy Edward ukipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jioni ya leo.
Ndugu jamaa na marafiki wa marehemu wakishusha mwili wa marehemu Willya Edward kwenye gari baada ya kuwasili katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kuhifadhiwa
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda akimfariji Kulwa Karedia mhariri wa magazeti ya Mtanzania ambaye alikuwa mmoja wa marafiki nda ndugu waliouleta mwili wa marehemu kutoka mkoani Morogoro.

Popular posts from this blog

CATHERINE MASUMBIGANA AWA REDD'S MISS CHANG'OMBE

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

HOTUBA YA MHESHIMIWA PEREIRA AME SILIMA (MB), MWENYEKITI WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI (T)