MKATABA

Serikali ya Tanzania na serikali ya Jamhuri ya watu wa China kesho (18/06/2012) zinatarajia kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa Bomba la kusafirisha Ges asilia kutoka Mnazi Bay Mtwara hadi Ubungo jijini Dar es Salaam.
Mkataba huo wenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 2 (mbili) utasainiwa mjini Beijing, China kati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini kwa upande wa Tanzania (TPDC) na Benki ya Exim kwa upande wa China.
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe Phillipo Marmo amesema hayo leo mjini Wuhan, China wakati akizungumza na Umoja wa Wanafunzi wa Tanzania (Wuhan Tanzania Students Association-UTASA) wanaoishi mjini hapo.
"Kesho Tanzania inatarajia kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Mnazi Bay Mtwara hadi Ubungo jijini Dar es Salaam utakaokamilika ndani ya mezi 12 baada ya kutiwa saini," amesema.
Kwa mujibu wa Balozi Marmo, "serikali ya Tanzania imeiwekea dhamana PTDC ili kupata mkopo kutoka benki ya Exim ya China."
ujenzi wa bomba hilo la gesi ni miongoni mwa jitihada za serikali kutatua kero ya umeme iliyodumu kwa muda mrefu kutokana na kupungua mara kwa mara kwa kina cha maji katika mabwawa yanyozalisha umeme yakiwemo Mtera na Kidatu ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo yanayo zalisha umeme unaotumika katika gridi ya Taifa.
"Mradi huu ukikamilika utasaidia kutatua kero ya umeme katika miji ya Dar es salaam. Arusha na kiasi kingine kitauzwa Nairobi nchini Kenya," amesema.
Pamoja na kutiliana saini mkataba huo, serikali hizo mbili hivi karibuni zimetiliana saini mkataba wa ujenzi wa nyumba 10,000 (elfu kumi) za askari jeshi nchini ili kupunguza tatizo la ukosefu wa makazi.
Balozi Marmo amesema, "Ujenzi wa nyumba hizi 10,000 ni mkopo wa riba nafuu kati ya asilimia 2 hadi moja utakaolipwa katika kipindi cha miaka 20."
Hata hivyo hakufafanua zaidi juu ya gharama za mradi huo. Mradi huo utajengwa na kamuni kutoka China.
China imekuwa mdau mkubwa wa miradi ya maendeleo nchini Tanzania tangu miaka ya 1960 na imejenga miradi mbalimbali ikiwemo TAZARA, Urafiki, Uwanja wa Taifa n barabara kadha.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA