Mashindano ya 126 ya Wimbledon yameanza


Li Na
Li Na aliondolewa mapema katika French Open lakini anatazamiwa kufanya vyema katika mapambano ya Wimbledon
Mashindano ya tennis ya Wimbledon nchini Uingereza yameanza Jumatatu, na kati ya wachezaji mahiri wanaoshiriki ni pamoja na Novak Djokovic kutoka Jamhuri ya Serbia, Maria Sharapova ambaye ni raia wa Urusi na Roger Federer kutoka Uswisi.
Waingereza saba pia wanashiriki katika mashindano ya mwaka huu.
Kati ya wachezaji ambao mambo yameanza kuwaendea vyema Jumatatu ni Mchina Li Na, ambaye moja kwa moja ameingia raundi ya pili ya mashindano, kwa kumuondoa Ksenia Pervak wa Kazakhstan 6-3, 6-1.
Baada ya kuondolewa mapema katika mashindano ya French Open katika raundi ya nne, Li Na inaelekea ameongeza juhudi za kufanya vyema katika mapambano ya Wimbledon.
Hata hivyo alionekana amemzidi nguvu Pervak, mwenye umri wa miaka 21, na alimuondoa haraka chini ya muda wa saa moja.
Sasa Li Na atakutana na Sorana Cirstea kutoka Romania, au Mfaransa Pauline Parmentier, katika raundi ya pili.

Popular posts from this blog

CATHERINE MASUMBIGANA AWA REDD'S MISS CHANG'OMBE

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

HOTUBA YA MHESHIMIWA PEREIRA AME SILIMA (MB), MWENYEKITI WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI (T)