IDARA
ya Habari ( MAELEZO) imetakiwa kujipanga vizuri ili kuweza kutekeleza
majukumu yake ya kuwa Msemaji wa Serikali ipasavyo; hatua hiyo
itasaidia kuepusha malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusiana na utendaji
wa Serikali.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Dkt. Fenella Mukangara wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Habari na
Mawasiliano wa Serikali katika ukumbi wa Victoria Palace Jijini Mwanza.
Aidha, Dkt. Mukangara
alisema, Idara ya Habari ( MAELEZO) ina jukumu zito la kuwa Msemaji
Mkuu wa Serikali . Hii ni kwa mujibu wa agizo la Serikali Na. C 16 la
mwaka 1977.
" Serikali inafanya
mambo mengi mazuri kwa wananchi lakini hayasemwi. Matokeo yake Serikali
inaishia kulaumiwa na wananchi bila sababu.
"Ndugu
zangu hali hii haikubaliki. Lazima tubadilike na lazima tuseme .
Hatuwezi kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali asiyesema." Alisema Dkt.
Mukangara.
Dkt. Mukangara
aliongeza kuwa Idara ya habari itekeleze jukumu hilo kwa kushirikiana na
Wasemaji wa Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali na Wasemaji hao
watambue kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ni Idara ya Habari.
Akizungumzia kuhusu
uhuru wa vyombo vya habari alisema,tunalo tatizo la baadhi ya vyombo vya
habari nchini kudhani kwamba uhuru wa vyombo vya habari hauna mipaka.
Hivyo alivitaka vyombo vya habari vitambue kuwa hakuna nchi yoyote
duniani ambayo utendaji wa vyombo vyake vya habri haubna mipaka.
" Wakati wote uhuru wa
vyombo vya habari popote pale huendana na wajibu hata ktika mataifa
yaliyoendelea"Alisema Dkt. Mukangara.
Aidha,
alivitaka vyombo vya habari kuwa makini katika kutangaza habari
zinazohusu mchakato wa mabadiliko ya katiba huku akisissitiza kuonyesha
uzalendo wa hali ya juu katika kuwahabarisha wananchi na kutoa elimu.