GAMBIA WAWASILI NCHINI
Timu
ya Taifa ya Gambia (The Scorpions) imewasili nchini jana (Juni 7 mwaka
huu) saa 5.30 usiku kwa ndege ya Kenya Airways tayari kwa ajili ya mechi
dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Msafara
wa timu hiyo wenye watu 31 wakiwemo wachezaji 22 unaongozwa na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana na Michezo wan chi hiyo, Malang Jassey.
Viongozi
wengine ni Ofisa Utawala wa timu Modou Sowe, Kocha Luciano Machini,
makocha wasaidizi Peter Bonu Johnson na Lamin Sambou, Kocha wa makipa
Alhagie Marong, mtaalamu wa tiba mbadala (physiotherapist) Pa Matarr
Ndow, Mtunza vifaa Sanna Bojang na Daktari wa timu Kalifa Manneh.
Wachezaji
ni Musa Camara, Abdou Jammeh, Momodou Futty Danso, Lamin Basmen
Samateh, Ousman Koli, Pa Saikou Kujabi, Mustapha Kebba Jarju, Yankuba
Mal Ceesay, Demba Savage, Saihou Gassama, Alieu Darboe, Momodou Ceesay,
Pa Modou Jagne, Tijan Jaiteh, Bubacarr Sanyang, Christopher Allen, Musa
Yaffa, Sulayman Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry, Ali Sowe, Omar Colley na
Saloum Faal.
Gambia
‘The Scorpions’ itafanya mazoezi yake ya kwanza leo (Juni 8 mwaka huu)
saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume wakati kesho muda huo
huo itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa.
Kambi
ya Taifa Stars iko vizuri ambapo leo jioni timu itafanya mazoezi Uwanja
wa Taifa. Pia kesho itafanya mazoezi kwenye uwanja huo huo kuanzia saa
11 jioni baada ya Gambia kuwa wamemaliza.
Jumamosi
saa 4 kamili asubuhi kutakuwa na mkutano kati ya makocha wa timu zote
mbili; Mdenmark Kim Poulsen wa Taifa Stars na Mtaliano Luciano Machini
wa The Scorpions wakiwa na manahodha wao na Waandishi wa Habari
utakaofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
TIKETI KUANZA KUUZWA JUMAMOSI
Tiketi
kwa ajili ya pambano la Taifa Stars na The Scorpions zitaanza kuuzwa
kesho (Juni 9 mwaka huu) kuanzia saa 2 asubuhi kwenye vituo vya Mgahawa
wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Shule ya Sekondari Benjamin
Mkapa, Soko Kuu la Kariakoo na Uwanja wa Taifa.
Pia
mauzo yatafanyika siku ya mechi kwenye vituo hivyo kuanzia saa 2
asubuhi hadi saa 6 mchana kabla ya kuhamia Uwanja wa Taifa.
Viingilio
katika mechi hiyo vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya rangi ya bluu na
kijani ambavyo ni 36,693 kati ya jumla ya viti 57,558 vilivyopo katika
uwanja huo wa kisasa. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa ni sh.
5,000.