MKE WA WAZIRI MKUU ATUNUKIWA SHAHADA NA MALECELA

Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, John Samwel Malecela akimtunuku Shahada ya Uongozi wa Biashara, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda katika Mahafali ya Chuo Kikuu Huria yaliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo hicho Kibaha Oktoba 27, 2012.Kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akipokea zawadi ya ua kutoka wadogo zake Salma Rehani (kulia), Mkaroga Rehani (wapili kulia) na Mabe Rehani baada ya kutunukiwa Shahada ya Uongozi wa Biashara katika mahafali ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika kwenye vianja vya Chuo hicho, Kibaha Oktoba 27, 2012 ( Picha Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akiwa na baadhiimu wa mahafali hayo yaliyofanyika jana Kibaha mkoani Pwani
Baadhi ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania Wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipowahutubia kwenye mahafali ya Chuo hicho yaliyofanyika Kibaha, Oktoba 27, 2012. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpongeza, Papius Yachitwi  ambaye alitunukiwa BA in Linguistic katiak Mahafali ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika kwenye  vianja vya Chuo hicho, Kibaha Octoba 27, 2012. Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho, John Samwel Malecela. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA