DK BILAL AFUNGA MAONESHO YA NANENANE DODOMA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mmoja kati ya wajasiliamali wa vikundi vya wakulima, wakati alipokuwa akifunga rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyomalizika leo Agosti 8, 2012 katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili wakati walipowasili kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma leo Agosti 8, 2012 kwa ajili ya kufunga rasmi maonyesho hayo .Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipomwakilisha Rais Jakaya Kikwete, kufunga rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyomalizika leo Agosti 8, 2012 katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha Tuzo aliyokabidhiwa kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa Rais katika kusimamia na kuendeleza Kilimo Kwanza, wakati Makamu alipokuwa akifunga rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma leo Agosti 8, 2012. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza. Picha na Muhidin Sufiani-OMR ( kwa hisani ya kamanda wa matukio blog )