RAIS KIKWETE ATEMBELEA SHAMBA LA MFANO LA KIJIJI CHA KICHOPELO,BAHI,MKOANI DODOMA

Rais Dkt .Jakaya Mrisho Kikwete akikagua  nyanya  na mazo mengine ya mboga pamoja na mizabibu katika shamba linalomilikiwa na kampuni ya kilimo ya Tendaji Trade huko katika kijiji cha Chikopelo,wilaya ya Bahi, Mkoani Dodoma  leo asubuhi.Kushoto ni mmoja wa wamiliki wa Shamba hilo Bwana Alon Hoven anayeshirikiana na Bwana Dunstan Mrutu(hayupo pichani).shamba hilo linamwagiliwa kwa kutumia teknolojia ya  matone(Drip irrigation system).
Mmoja wa Wamiliki wa Shamba la Mboga katika kijiji cha Chikopelo Bwana Alon Hoven kimwonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete baadhi ya mazao yanayozalishwa kwa kutumia mbegu bora pamoja na teknolojia ya ya umwagiliaji wa matone wakati Rais alipotembelea shamba hilo katika kijiji cha Chikopelo, wilayani Bahi,mkoani  Dodoma leo asubuhi.Shamba hilo lenye ukubwa wa hekari mia moja linamilikiwa na kampuni ya kilimo ya Tendaji Trade chini ya Bwana Dunstan Mrutu na Alon Hoven raia wa Israel.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Rais Kikwete alisifu juhudi za wawekezaji hao kwa kutumia mbinu za kisasa za kilimo na kuwaasa wanakijiji wa Chikopelo kujifunza mbinu bora za kilimo hicho cha mboga ili waweze kupata ufanisi na kuboresha maisha yao. Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kuwaonya viongozi wa kijiji cha Chikopelo kutoendelea kuuza ardhi yote kwa wawekezaji na badala yake kutunza na kuilinda kwaajili ya kizazi kijacho.
Awali katika salamu zao kwa Rais,Bwana Dunstan Mrutu  na mmiliki mwenzake bwana Alon Hoven mbali na kutoa ajira kwa wanakijiji hao waliahidi kushirikiana nao katika kujifunza mbinu bora za kilimo na kuwawezesha kuzalisha mazao bora na mengi

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA