MKUU WA MKOA WA ARUSHA

Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa mulongo
Na Ashura Mohamed,Arusha
VIONGOZI wa serikali pamoja na wa madhehebu ya dini wametakiwa kutambua kuwa wana wajibu mkubwa wa kubadili mitazamo na imani kwa wananchi wao wanaowaongoza ikiwa ni pamoja na kuwa wawazi na wawajibikaji ili pawe na utawala bora katika jamii.

Hayo yalisemwa na mkuu wa wilaya ya mbeya Dk Norman Sigala wakati alipokuwa akiongea katika mdahalo wa umma unahousu uwazi na uwajibikaji wa viongozi na watendaji wa serikali katika kusimamamia rasilimali za umma uliandaliwa na muungano wa asasi za kiraia( Angonet) na kufanyika mjini hapa.

Alieleza kuwa ni vema viongozi wakawa na maadili na wakahakikisha kuwa wanatenda haki kwa wananchi wao kwa kuwa wawazi kwa mambo mbali mbali wanayoyafanya ili kuwaepusha na migogoro mbali mbali inayotokea baina yao na wananchi.

“Endapo viongozi watakuwa wawazi kuwaeleza wananchi wao mambo yanayoendelea katika halmashauri zao itasaidia kuelewa matatizo na mafaniko yaliopo ndani yao hivyo kufanya kuepukana na malumbano yasiyokuwa na tija”alisema Sigala.
Awali mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa mkoa katibu tawala msaidizi utawala na rasilimali mkoa wa Arusha Jacob Mwanga alisema kuwa uwajibikaji wa viongozi na watendaji wa serikali kwa wananchhi ni muhimu katika kuboresha utendaji wa serikali kuu na za mitaa hali itayopelekea kuendeleza na kukuza utawala wa sheria.

Alisema kuwa ili viongozi wawe wawazi na wawajibikaji kwa wananchi wao wanapaswa kuacha vitendo vya ubadhirifu na ukosefu wa maadili kwa kuwa hivi ndivyo baadhi ya vitu vinavyowanyima kuwa wazi kwa wananchi wao

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA