BENKI YA CRDB YAFANIKIWA KUONGEZA MIKOPO KWA ASILIMIA 27


BENKI ya CRDB  imefanikiwa kuongeza  utoaji wa mikopo yake  kwa
asilimia 27,  kufikia  shilingi bilioni 1.4  kutoka  shilingi bilioni
1.1 mwaka 2010.

Hayo yalisemwa  na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB nchini, Dk.Charles Kimei, wakati alipokuwa akizungumza kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa kumi na saba wa wanahisa wa benki hiyo uliofanyika  Jijini Arusha.
 Aidha sekta ya kilimo   imeongoza kwa kuchangia  asilimia 30 ya mikopo yote  iliyotolewa na benki hiyo, huku ikifuatiwa na  biashara na viwanda kwa asilimia 14.
Pia alizitaja sekta zingine ambazo zimechangia  ukuaji wa mikopo hiyo kuwa ni mikopo binafsi asilimia 12, Utalii, hoteli na migahawa asilimia 8, wakala wa masuala ya kifedha  asilimia 7,upangishaji majengo na ujenzi 6, mawasiliano na uchukuzi  kila moja asilimia 7. huduma za kijamii 6, uzalishaji na usindikaji 3 na uchimbaji wa madini na kokoto  asilimia 1.
Lakini hata hivyo alisema ukuaji huo umechangiwa  na chapa ya Benki , ambayo  imeendelea kuboreshwa kwa kampeni za masoko, kuanzishwa na kubuniwa kwa bidhaa na huduma mpya,kukua na kusambaa kwa njia za utoaji  huduma.

Pia alisema pamoja na changamoto za uchumi zilizoikumba biashara na Benki,utendaji katika maeneo mengi umekuwa wa kuridhisha, kwa kuongeza ukopeshaji ambapo waliweza kuongeza pato lake la riba huku ikipunguza gharama za riba, kiasi cha kuzalisha pato halisi la riba la shilingi bilioni 157.4 ikilinganishwa na shilingi bilioni 125 kw amwaka uliopita.

Dk. Kimei alisema kuwa benki yao imejikita zaidi katika uwekezaji katika jamii na udhamini kwa kutazama vipaumbele vya jamii, ambavyo ni elimu, afya na mazingira huku nguvu kubwa ikielkezwa katika makundi yaliyosahauliwa katika jamii na kuchangia wahanga wa majanga yaliyoikumba nchi ndani ya mwaka 2010.

Alisema  benki hiyo hadi kufikia sasa, wana mtandao wa matawi 82 ikiwa pamoja na matawi yanayotembea, kwa angalau tawi moja, katika kila Mkoa nchi nzima na wana mtandao (Internet)  wa huduma za benki, ambazo zinawafikia wateja 20,000 na huduma inayokua haraka kupitia simu ya
mkononi ikiwa na zaidi ya wateja 30,000, kufikia mwishoni mwa Desemba
2011.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA