RAIS KIKWETE ATEMBELEA SHAMBA LA MFANO LA KIJIJI CHA KICHOPELO,BAHI,MKOANI DODOMA
Rais Dkt .Jakaya Mrisho Kikwete akikagua nyanya na mazo mengine ya mboga pamoja na mizabibu katika shamba linalomilikiwa na kampuni ya kilimo ya Tendaji Trade huko katika kijiji cha Chikopelo,wilaya ya Bahi, Mkoani Dodoma leo asubuhi.Kushoto ni mmoja wa wamiliki wa Shamba hilo Bwana Alon Hoven anayeshirikiana na Bwana Dunstan Mrutu(hayupo pichani).shamba hilo linamwagiliwa kwa kutumia teknolojia ya matone(Drip irrigation system). Mmoja wa Wamiliki wa Shamba la Mboga katika kijiji cha Chikopelo Bwana Alon Hoven kimwonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete baadhi ya mazao yanayozalishwa kwa kutumia mbegu bora pamoja na teknolojia ya ya umwagiliaji wa matone wakati Rais alipotembelea shamba hilo katika kijiji cha Chikopelo, wilayani Bahi,mkoani Dodoma leo asubuhi.Shamba hilo lenye ukubwa wa hekari mia moja linamilikiwa na kampuni ya kilimo ya Tendaji Trade chini ya Bwana Dunstan Mrutu na Alon Hoven raia wa Israel. Akizungumza wakati wa ziar...