Posts

Showing posts from June 24, 2012

I DID NOTHING WRONG

Image
Deputy Minister for Communications, Science and Technology,  Hon January Makamba --- *I did nothing wrong as deputy minister to instruct TCRA I read with particular interest an article published in the May 25 edition of this newspaper titled ‘Collective responsibility and emerging anarchy in state policy’ by Ani Jozeni. The article would not have warranted a response if it were not so elegantly written, so blatantly misleading and wrong on both facts and logic. I am taking the liberty to respond so as to correct certain factual errors and flaws in logic, and offer him and the readers a bit of understanding about the telecoms sector. Jozeni’s gripe is twofold: one, that it was incorrect for a government leader to ask Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) to take up with mobile phone operators an issue about poor mobile phone services and that we, who do not reside at the Treasury, must not complain about poor tax revenue collection fr...
Image
Safari ya mwisho ya mpiganaji Willy Edward kijijini kwao Molotonya   Waombolezaji wakiwa katika msiba wa marehemu Willy Edward nyumbani kwao  Molotonga, Mugumu Mjini, Serengeti, mkoani Mara, leo   Waombolezaji wakiwa wamejipanga foleni tayari kwenda ktuo heshima za   mwisho kwa mwili wa marehemu Willy Edward.   Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Absalom Kibanda (katikati),   akiwaongoza baadhi ya wahariri kuweka shada la maua katika kaburi la   marehemu Willy Edward wakati wa maziko yaliyofanyika Molotongo, Mugumu.   Baba wa marehemu Willy Edward, Edward Ogunde akilia baada ya kutoa   heshima za mwisho kwa nmwili wa mwanawe   Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja akitoa heshima za mwisho   kwa mwili wa marehemu Willy Edward.   Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jacquiline Liana akitoa heshima za mwisho kwa mwili   wa marehemu Willy Edward nyumbani kwao marehemu Molotonga, Mugumu ...

Fernando Alonzo ashinda Langalanga Ulaya

Image
Dereva wa magari ya Timu ya Ferrari Fernando Alonso amekua dereva wa kwanza kushinda mara mbili mwaka huu kwa ushindi wa kishindo kwenye mashindano ya Ulaya. Fernando Alonso Yeye Alonzo alianza katika nafasi ya 11 kabla ya gari la usalama kuingilia mashindano kufuatia ajali lakini juhudi zake zilimuezesha kupambana hadi nafasi ya nne. Aliweza kuongoza kufuatia mizengwe iliyotokea ndani ya kituo cha magari ya McLaren ambako wakati wa kubadili tairi na kuongezea mafuta Hamilton alipoteza zaidi ya sekundi 14 na kwa bahati nzuri dereva aliyekua akiongoza Sebastien Vettel akashindwa kumaliza mbio hizo. Ferrari la Alonso Kimi Raikkonen alimaliza wa pili, il hali Hamilton akikwama ikisalia mizunguko miwili baada ya kukwaruzana na Pastor Maldonaldo wa timu ya magari ya Williams. Hadi hapo ...

TANZANIA NA CHINA ZAJIVUNIA MAFANIKIO YA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA SHUGHULI ZA KILIMO.

Image
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza (kulia) akizungumza jambo na Balozi wa China nchini Tanzania Bw.Lu Youqing wakati wa hafla fupi ya kusherehekea    mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya  China na Tanzania kwenye miradi mbalimbali ya kilimo nchini. Viongozi mbalimbali kutoka ubalozi wa China na seraikali ya Tanzania wakiimba wimbo wa Taifa wa Tanzania kabla ya kuanza   hafla fupi ya kusherehekea    mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya  China  na Tanzania kwenye miradi mbalimbali inayofanyika nchini Tanzania.Kutoka kushoto nyuma ni balozi wa China nchini Tanzania Bw.Lu Youqing, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule. Baadhi ya mashuhuda wa miradi mbalimbali ya ushirikiano kati ya Chin...

PRECESION AIRWAYS YAFIKA ZAMBIA

Image
 Mkurugenzi Mkuu na CEO wa Precision Air, Alfonse Kioko akizungumza wakati wa tafrija ya uzinduzi wa safari za Shirika hilo la ndege jana kutoka Dar es Salaam hadi Lusaka Zambia kupitia Lubumbash.Hafla hiyo iliyofanyika katika mji wa Lusaka Hoteli ya Taji Pamodz.  Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Grace Mujuma akizungumza wakati wa uzinduzi huo.   Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Uchukuzi, John Thomas James Mngodo akizungumza kaatika hafla hiyo iliyofanyika katika mji wa Lusaka Hoteli ya Taji Pamodz. Mgeni Rasmi, Naibu Wazizi wa Usafirishaji, Kazi, Usambazaji na mawasiliano wa Zambia, Samuel Mukupa akizungumza jana katika tafrija maalum ya uzinduzi wa safari za Ndege za Kampuni ya Precision Air kutoka Dar es Salaam kwenda Lusaka kupitia Lubumbashi. Mukupa alisema mbali ya kuzidisha mahusionao baina ya Tanzania na Zambia lakini pia itawasaidia sana wafanya biashara wa Zambia katika safari zao za kibiashara Tanzania. Wageni mbali...

Marekani yaonya kutatokea ugaidi Kenya

Image
Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umeonya kwamba kuna tishio la shambulio la kigaidi kutokea mjini Mombasa karibuni, na umewataka watumishi wa serikali ya Marekani kuondoka katika mji huo. Hii siyo mara ya kwanza kwa onyo kama hilo kutolewa. Mwezi wa Oktoba mwaka jana, ubalozi wa Marekani ulisema kuna tishio la shambulio kwenye maeneo ambayo hutembelewa na wageni kama vile maeneo ya maduka mengi na vilabu vya starehe. Wakati huo hakuna lilotokea, lakini hali katika nchi ya jirani, yaani Somalia, imezidisha wasiwasi. Marekani imehusika na mapambano dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu wa Somalia, ambao baadhi yao wana maingiliano na jamii kubwa ya Wasomali inayoishi Kenya. Marekani haitaki kupita tena kwenye maafa ya mwaka wa 1998, ambapo ubalozi wake mjini Nairobi ulishambuliwa kwa mabomu, na watu zaidi ya 200 walikufa...

BENKI YA CRDB YAFANIKIWA KUONGEZA MIKOPO KWA ASILIMIA 27

Image
BENKI ya CRDB  imefanikiwa kuongeza  utoaji wa mikopo yake  kwa asilimia 27,  kufikia  shilingi bilioni 1.4  kutoka  shilingi bilioni 1.1 mwaka 2010. Hayo yalisemwa  na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB nchini, Dk.Charles Kimei, wakati alipokuwa akizungumza kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa kumi na saba wa wanahisa wa benki hiyo uliofanyika  Jijini Arusha.  Aidha sekta ya kilimo   imeongoza kwa kuchangia  asilimia 30 ya mikopo yote  iliyotolewa na benki hiyo, huku ikifuatiwa na  biashara na viwanda kwa asilimia 14. Pia alizitaja sekta zingine ambazo zimechangia  ukuaji wa mikopo hiyo kuwa ni mikopo binafsi asilimia 12, Utalii, hoteli na migahawa asilimia 8, wakala wa masuala ya kifedha  asilimia 7,upangishaji majengo na ujenzi 6, mawasiliano na uchukuzi  kila moja asilimia 7. huduma za kijamii 6, uzalishaji na usindikaji 3 na uchimbaji wa madini na kokoto  asili...

RAIS KIKWETE AKIKAGUA MRADI WA KUFYATUA MATOFALI NA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA MBOGA

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua matofali yaliyotengenezwa kwa mashine ya Hydrafoam kwaajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari ya Mboga,wilayani   Bagamoyo. Mashine   hiyo yenye thamani ya Shilingi Milioni Sabini 70m/- imetolewa na Rais Kikwete kama msaada kwa vijana waliounda ushirika ili kuboresha maisha yao kwa kufanya   miradi mbalimbali ya ujenzi na uzalishaji(picha na Freddy Maro)