BENKI YA CRDB YAFANIKIWA KUONGEZA MIKOPO KWA ASILIMIA 27
BENKI ya CRDB imefanikiwa
kuongeza utoaji wa mikopo yake kwa
asilimia 27, kufikia shilingi bilioni 1.4 kutoka shilingi bilioni
1.1 mwaka 2010.
asilimia 27, kufikia shilingi bilioni 1.4 kutoka shilingi bilioni
1.1 mwaka 2010.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB nchini, Dk.Charles Kimei, wakati alipokuwa akizungumza kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa kumi na saba wa wanahisa wa benki hiyo uliofanyika Jijini Arusha.
Aidha sekta ya
kilimo imeongoza kwa kuchangia asilimia 30 ya mikopo yote
iliyotolewa na benki hiyo, huku ikifuatiwa na biashara na viwanda kwa
asilimia 14.
Pia alizitaja sekta zingine ambazo
zimechangia ukuaji wa mikopo hiyo kuwa ni mikopo binafsi asilimia
12, Utalii, hoteli na migahawa asilimia 8, wakala wa masuala ya kifedha
asilimia 7,upangishaji majengo na ujenzi 6, mawasiliano na uchukuzi kila
moja asilimia 7. huduma za kijamii 6, uzalishaji na usindikaji 3 na uchimbaji
wa madini na kokoto asilimia 1.
Lakini hata hivyo alisema ukuaji huo
umechangiwa na chapa ya Benki , ambayo imeendelea kuboreshwa kwa
kampeni za masoko, kuanzishwa na kubuniwa kwa bidhaa na huduma mpya,kukua na
kusambaa kwa njia za utoaji huduma.
Pia alisema pamoja na changamoto za uchumi zilizoikumba biashara na Benki,utendaji katika maeneo mengi umekuwa wa kuridhisha, kwa kuongeza ukopeshaji ambapo waliweza kuongeza pato lake la riba huku ikipunguza gharama za riba, kiasi cha kuzalisha pato halisi la riba la shilingi bilioni 157.4 ikilinganishwa na shilingi bilioni 125 kw amwaka uliopita.
Dk. Kimei alisema kuwa benki yao imejikita zaidi katika uwekezaji katika jamii na udhamini kwa kutazama vipaumbele vya jamii, ambavyo ni elimu, afya na mazingira huku nguvu kubwa ikielkezwa katika makundi yaliyosahauliwa katika jamii na kuchangia wahanga wa majanga yaliyoikumba nchi ndani ya mwaka 2010.
Alisema benki hiyo hadi kufikia sasa, wana mtandao wa matawi 82 ikiwa pamoja na matawi yanayotembea, kwa angalau tawi moja, katika kila Mkoa nchi nzima na wana mtandao (Internet) wa huduma za benki, ambazo zinawafikia wateja 20,000 na huduma inayokua haraka kupitia simu ya
mkononi ikiwa na zaidi ya wateja 30,000, kufikia mwishoni mwa Desemba
2011.