Serengeti Fiesta 2012 yaanza kwa kishindo mjini Moshi
Wasanii machachari Bongo Move Wema Sepetu (kushoto) na Aunt Ezekiel wakicheza muziki wa bongo Fleva uliokuwa ukishushwa na Msanii wa Bongofleva,Ferooz katika uzinduzi wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 Bhaaaaass! katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi usiku huu. Tamasha hilo limebamba ile mbaya. Ferooz akiwa na mmoja wa mashabiki wake wakilishambulia jukwaa vilivyo. Sehemu ya wakazi wa mji wa Moshi wakiendelea kushuhudia makamuzi ya wasanii mbalimbali wanaotumbuiza usiku huu kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012. Prezoo akiwarusha mashabiki kibao (hawapo pichani) waliojitokeza jioni ya leo kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 Pichani juu na chini ni mwanamuziki kutoka nchini Kenya na mmoja wa shiriki wa shindano la Big Brother Stargame,CMB Prezoo akitumbuiza jukwaani usiku huu kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja wa chuo cha ushirika mjini Moshi. Mmoja wa wasanii w...