Posts

Showing posts from December 22, 2012

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa Azungumza na Waandishi wa Habari juu ya Vibali Vya Mazingira

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akiwaonyesha cheti cha Ukaguzi wa Mazingira ambacho hupatiwa Wamiliki wa Mahoteli na viwanda. Waziri Huvisa alikuwa akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini Kwake Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Cherles Kikwanga akitoa Ufafanuzi wa jambo wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt.Terezya Huvisa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akitoa Ufafanuzi wa Vibali vya Mazingira kwa Mwandishi wa Gazeti la Jambo Leo Bw. Peter Ambilikile wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari leo Ofisini kwa Waziri Mtaa wa Luthuli Mijni Dar es Salaam.Picha na Ali Meja-Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira

KARIBU

Image
MSTAHIKI MEYA JERRY SILAA ASHIRIKI IBADA MAALUM NA JUMUIYA YA SHREE SANATAN DHARMA SABHA KULIOMBEA TAIFA AMANI. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wahindu Tanzania Bw. Ramesha Patel akimpokea na kumtambulisha mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wakati alipowasili kwenye msikiti mkuu wa Dhehebu hilo ulioko jijini Dar es Salaam kwa shughuli maalum ya kuliombea taifa Amani. Mstahiki Meya Jerry Silaa akilakiwa na kuvishwa shada la maua. Mstahiki Meya Jerry Silaa akiingia katika msikiti wa dhehebu la Wahindu kuhudhuria ibada maalum ya kuliombea taifa Amani. Waendesha Ibada maalum kutoka India katika moja ya hatua za ibada hiyo wakimpa baraka za namna ya pekee Mstahiki Meya Jerry Silaa. Mstahiki Meya Jerry Silaa akishiriki kuomba dua na waumini wa dhehebu hilo. Mstahiki Meya Jerry Silaa katika hatua nyingine ya ibada hiyo akizungushwa ndani ya msikiti huo. Waumini wa dhehebu la Hindu wakiwa wamekusanyika katika sehemu maal...

JESHI LA POLISI LATOA SIKU SABA KWA BAADHI YA ASKARI POLISI WANAODAIWA KUIBA MILIONI 150 ZILIZOPORWA

Image
           JESHI la Pol i si l imeto a siku saba kwa baadhi ya aska ri kuzisalimisha  fedha zipatazo sh milioni 150 wanazodaiwa kuiba, ambazo zilizoporwa na majambazi Mtaa wa Mahiwa na Livingston jijini Dar es Salaam juzi. Akizungumza na waandishi wa habari jijini, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova, alisema kutokana na tuhuma hizo jeshi hilo limeunda Jopo la wapelelezi ili kujua ukweli wa madai hayo. Alisema Jopo hilo litaundwa na watu watano, likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum, Ahmed Msangi, atakayehakikisha kwamba muda mfupi inavyowezekana, ukweli upatikane ili wananchi wajulishwe matokeo. Kamanda Kova alisema jeshi hilo lina mfumo wake wa kuchunguza askari wake inapotokea amejihusisha katika matukio yanayokwenda kinyume na maadili ya kazi yake