MSAADA KWADELO
Mama Maria akimkabidhi funguo za trekta moja kati ya kumi aliyokabidhi, mmoja wa wakulima hao Sheikh Hamis Haji ambaye pia ni Sheikh wa Kata ya Kwadelo . Mkazi wa kijiji cha Kwadelo, Maulid Msema akipokea funguo moja kati ya 10 za Matrekta yaliyokabidhiwa na Mama Maria Nyerere kwa ajili ya wakulima wa kijiji hicho kilichopo wilayani Kondoa, kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kilimo kijijini hapo, katika hafla iliyofanyika Msasani jijini Dar es Salaam jana. Kushoto anayeshuhudia ni Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omari Kariati. Kisha Kariati akamkabidhi zawadi ya Kitenge Mama Nyerere kama shukurani ya wananchi wa Kwadelo kujengewa kisima cha maji na baba wa Taifa Mwalimu mwaka 1961 ambacho hadi sasa kipo. Halafu akamkabidhi mkoba wa safari kama akitaka kwenda Butiama kijijini kwake Omary Kariati diwani wa kata ya kwadelo,wilayani kondoa mkoa wa Dodoma akizungumza neno la kufungua shughuli. Kulia ni M...