Kombaini ya Copa Coca-Cola Tanzania (Dream Team) yenye wachezaji 16 inatarajia kuondoka kesho (Agosti 28 mwaka huu) asubuhi kwenda Afrika Kusini kwenye kambi itakayokuwa chini ya makocha wa Chelsea. Makocha watano kutoka timu ya Chelsea ya Uingereza ndiyo watakaoongoza kambi maalumu ya kimataifa ya Copa Coca-Cola yenye wachezaji 140 kutoka nchini 15 itakayofanyika jijini Pretoria kuanzia Agosti 28 hadi Septemba 8 mwaka huu. Robert Luke Udberg, Russel William Banyard, Oliver Staurt Woodall, Shane Jason Hughes na Dean Aaron Steninger kutoka Chelsea FC Foundation ndiyo wanaounda jopo hilo la makocha litakalowanoa vijana hao wenye umri chini ya miaka 17. Wachezaji wanaounda Dream Team iliyotokana na michuano ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 24 hadi Julai 15 mwaka huu ni Abrahman Said Mohamed (Zanzibar), Ayubu Alfan (Dodoma), Baker Hamad (Tanga), Edward Joseph (Ruvuma), Hassan Kabunda (Temeke) na Jos...