Wahamiaji 42 wafa kwenye lori Tanzania
Tanzania Wahamiaji haramu arobaini na wawili wamepatikana wakiwa wamekufa ndani ya lori walimokuwa wakisafiria katika mkoa wa Dodoma, nchini Tanzania. Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania, Pereira Silima, amesema kuwa watu hao waliokuwa wamesongamana ndani ya lori waliaga dunia kutokana ukosefu wa hewa safi. ''Taarifa tuliyopata ni kwamba kulikuwa na wasafiri waliokuwa wakisafirishwa kwenye lori, ambalo lilikuwa kama kontena na halikuwa na hewa ya kutosha''.Bwana Silima ameambia BBC. wahamiaji walikuwa wanatoka Ethiopia Amesema wahamiaji hao haramu kutoka Ethiopia walikuwa wakijaribu kuingia Malawi. Kulingana na bwana Silima wahamiaji hao walianza kufariki dunia wakiwa safarini. Jihudi za wahamiaji hao kumjulisha dereva kuhusiana na hali yao hazikufanikiwa, na hivyo kusababisha maafa ya watu arobaini na moja ndani ya lori hilo. Kulingana na naibu waziri huyo wa mambo ya ndani tukio hilo lilifanyika Jumatatu usiku. Na ba...