AMSHA AMSHA LA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012 MOSHI MJINI

Mtangazaji wa kipindi cha Amplifaya kutoka Clouds FM akizungumza na mmoja wa mashabiki wa kituo hicho cha redio,mapema leo mtaa wa Ghala mjini Moshi,ikiwa ni sehemu ya mchakato mzima wa amsha amsha ya tamasha kubwa la Serengeti Fiesta,ambalo linatarajiwa kufanyika mjini humo siku ya ijumaa katika chuo cha ushirika.wasanii watakao shiriki kadhaa ni Joh Makini,Mwana FA,Linah,Godzilla,Juma Nature,Ommy Dimpoz,Bob Junior,Sheta,Ferooz,Richard Mavoko,washindi wa Supa Nyota na wengineo kibao. Kama vile haitoshi kutakuwepo na wasanii lukuki wa bongofleva akiwemo na aliyeshiriki shindano la Big Brother Stargame,CMB Prezzoo. Washkaji nao hawataki kupitwa kabisa na shughuli nzima ya mambo yanayoshushwa na Clouds FM,hapa walikuwa wakisikiliza kipindi cha amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 lililokuwa likirushwa live hewani ndani ya mji wa Moshi mapema leo mtaa wa Ghala. Kiongozi wa msafara wa amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 mjin...