AMSHA AMSHA LA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012 MOSHI MJINI
Mtangazaji
wa kipindi cha Amplifaya kutoka Clouds FM akizungumza na mmoja wa
mashabiki wa kituo hicho cha redio,mapema leo mtaa wa Ghala mjini
Moshi,ikiwa ni sehemu ya mchakato mzima wa amsha amsha ya tamasha kubwa
la Serengeti Fiesta,ambalo linatarajiwa kufanyika mjini humo siku ya
ijumaa katika chuo cha ushirika.wasanii watakao shiriki kadhaa ni Joh
Makini,Mwana FA,Linah,Godzilla,Juma Nature,Ommy Dimpoz,Bob
Junior,Sheta,Ferooz,Richard Mavoko,washindi wa Supa Nyota na wengineo
kibao.Kama vile haitoshi
kutakuwepo na wasanii lukuki wa bongofleva akiwemo na aliyeshiriki
shindano la Big Brother Stargame,CMB Prezzoo.
Washkaji
nao hawataki kupitwa kabisa na shughuli nzima ya mambo yanayoshushwa na
Clouds FM,hapa walikuwa wakisikiliza kipindi cha amsha amsha ya tamasha
la Serengeti Fiesta 2012 lililokuwa likirushwa live hewani ndani ya mji
wa Moshi mapema leo mtaa wa Ghala.
Kiongozi
wa msafara wa amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 mjini
Moshi,Dj Mully B akiendelea kuweka mambo sawa kwenye gari yao ya
matangazo ya live (OB-Van) kabla ya kuanza kuruka live,kati ni Eric
Kusaga sambamba na Simon Malenga wakifuatilia kwa ukaribu kuhakikisha
kila kitu kinakwenda.
Mmoja
wa mashabiki damu wa Clouds FM akimuelekeza Millard Ayo shughuli zao
mbalimbali wanazozifanya ikiwemo na namna wanavyoupanda mlima
kilimanjaro wakiwa na wageni wao mbalimbali,hapa alikuwa akimuonesha
sehemu ya Mlima Kilimanjaro uliokuwa uking'ara vizuri kabisa.
Haa haaa ni wakati wa msimu si vibaya ukajivunia.
Aaahh...jamaaani
wewee ndio Millard Ayo..! yule anaetangaza kipindi cha Amlifaya Clouds
FM..! wwooowww....! nafurahi kukuona,so how are u..!
Millard
Ayo akiendelea na amsha amsha yake ya tamsha la Serengeti Fiesta kwa
wadau mbalimbali mapema leo ndani ya mji wa Moshi,ambapo katika
muendelezo wa tamasha hilo zimepangwa kutolewa zawadi kede kede,ikiwemo
simu za mikononi,piki piki,fedha taslim na nyinginezo kibao,huku zawadi
kubwa ikiwa ni ya gari aina ya Vits.
Kiongozi
wa msafara wa amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 mjini
Moshi,Dj Mully B akitoa maelekezo mafupi namna ya kujishindia zawadi
mbalimbali za Serengeti Fiesta kwa mdau wa Clouds FM.

Vijana
mbalimbali waliojitokeza maeneo ya mtaa Ghala,jijini Moshi wakati wa
amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012,ambapo washabiki
mbalimbali walijipatia fulana za Fiesta,tayari kwa kwenda kujiachia siku
ya ijumaa ambapo tamasha hilo litakaporindima ndani ya chuo cha
ushirika,ambapo kiingilio kimepangwa kuwa ni sh 5000 kwa kila
mmoja,tamasha hilo baada ya kurindima mkoni Moshi pia litahamia mjini
Tanga katika uwanja wa Mkwakwani siku ya jumapili.