BAADHI ZA PICHA KATIKA TUKIO LA GHOROFA LILILOPOROMOKA ASUBUHI HII YA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.
Kamanda wa Kanda maalum ya Kipolisi mkoa wa Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova kulia akizungumza jambo na Mbunge wa kuteuliwa Mh. James Mbatia ambaye ameungana na wananchi wengine katika tukio hilo. Uokoaji ukiendelea katika eneo la tukio. Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick akiwa katika eneo la tukio kusimamia zoezi la uokoaji. Ulinzi ukiwa umeimarishwa katika eneo la tukio Kibao hiki kinaonyesha kampuni ambazo zilikuwa zikijenga jengo hilo. Kijiko kikiendelea kuondoa kifusi katika eneo la tukio Wananchi wakishiriki katika zoezi la uokoaji kwa kuondoa taka na vifusi katika eneo hilo.