Mbunge wa CUF, Jimbo la Chambani Pemba Salim Hemed Khamis Afariki Dunia,Kuagwa leo, Asubuhi Viwanja Vya Karimjee Jijini Dar es Salaam Kuzikwa Pemba
Mbunge wa CUF, Jimbo la Chambani Pemba kisiwani
Zanzibar, Marehemu, Salim Hemed
Baadhi ya Maofisa wa Ofisi Ndogo ya Bunge,wakimsaidia kwa kumbeba Mbunge wa Chambani,Bwa.Salim
Hemed Khamis,mara baada ya kuanguka ghafla hapo juzi jijini Dar akiwa
katika vikao vya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu ya haraka.
--
MAZISHI ya aliyekuwa Mbunge wa CUF, Jimbo la Chambani Pemba kisiwani
Zanzibar, Marehemu, Salim Hemed Khamis,yanataraji
kufanyika leo mchana mjini Pemba.
Taarifa za awali kutoka Chama cha Wananchi CUF, zinasema kuwa Mwili wa Marehemu,
Khamis utaagwa leo asubuhi kuanzia majira ya saa 2:30-4:00 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es
Salaam ambapo Viongozi mbalimbali wa kitaifa na Kimataifa pamoja na wananchi na
Wanachama wa CUF watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu.
Taarifa hiyo ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julis Mtatiro inasema kuwa
Msafara utaondoka Karimjee saa 4:00 kuelekea uwaja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere ambapo Msafara wa Ndege 2 utaondoka kwenda Pemba.
Saa saba mchana mazishi yatafanyika huko Pemba na maazishi hayo
yataongozwa na Viongozi wa serikali, Wabunge na CUF.