
Said Bahanuzi ni mshambuliaji mahiri wa timu ya Yanga ya nchini Tanzania jana alithibitisha kwamba yeye ni mchezaji halali wa Yanga na ataendelea kuwa mchezaji wa Yanga kwa muda wa miaka miwili kwa tamko hilo Bahanuzi ameondoa utata uliokuwa unaanza kuvuma jijini Dar Es Salaam na nchi kwa ujumla kwamba huenda mchezaji huyo amehamia timu pinzani ya Simba ambao haikufanya vizuri katika mashindano ya hivi karibuni ya Kagame Cup iliyoshirikisha timu mbali mbali za klabu za afrika mashariki na kati na ikiwemo kuiwakilisha timu ngeni ya kutoka Congo ya Vita FC ingawa timu hiyo ilishika nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo.