Posts

Showing posts from December 24, 2012

Meya Jerry Silaa ashiriki katika kampeni ya Usafi Katika Kata ya Gongo la Mboto.

Image
  Pichani Juu na Chini ni Mstahiki Meya wa Ilala na Diwani wa Kata ya Gongo la mboto, Jerry Silaa akiwa na baadhi ya  wakazi wa Kata hiyo wakifanya kazi ya usafi katika eneo la Stendi ya Mabasi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhimiza usafi na kuhifadhi mazingira katika jiji la Dar es Salaam iliyozinduliwa na makamu wa Rais mwanzoni mwa mwezi huu. Mstahiki Meya wa Ilala na Diwani wa Kata ya Gongo la mboto,Jerry Silaa akizungumza na baadhi ya  wakazi wa Kata hiyo wakati wa kufanya usafi katika eneo la Stendi ya Mabasi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhimiza usafi na kuhifadhi mazingira katika jiji la Dar es Salaam iliyozinduliwa na makamu wa Rais mwanzoni mwa mwezi huu

Mechi kati ya Taifa Stars na Chipolopolo ya Zambia yaingiza Tsh. Mil 109/-.

Image
  Pambano la kirafiki la kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zambia (Chipolopolo) lililochezwa juzi (Desemba 22 mwaka huu) limeingiza sh. 109,197,000. Fedha hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 17,383 waliokata tiketi kushuhudia mechi kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 16,657,169.49, maandalizi ya mchezo sh. 55,339,510, tiketi sh. 5,803,900, ulinzi na usafi kwa Uwanja wa Taifa sh. 2,350,000, Wachina (technical support) sh. 2,000,000, umeme sh. 300,000 na maandalizi ya uwanja (pitch marking) sh. 400,000. Nyingine ni bonasi kwa Taifa Stars sh. 13,826,313, asilimia 20 ya gharama za mchezo sh. 2,504,022, asilimia 10 ya uwanja sh. 1,252,011, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 626,005 na asilimia 65 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 8,138...
Image