Posts

Showing posts from August 23, 2012

MCHAKATO WA SERENGETI FIESTA 2012 WAENDELEA KUPAMBA MOTO NDANI YA JIJI LA TANGA

Image
  Mchakato wa Serengeti Fiesta 2012 ndani ya Tanga ukiendelea ndani ya mitaa kadhaa ya jiji hili. Mtangazaji wa Clouds Fm Adamu Mchomvu, hapa vijana wa kazi kutoka Clouds Fm wakiongea na wakazi wa eneo la Magaoni, Taili Tatu Kata ya Mabawa. Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 26.8.2012 katika uwanja wa Mkwakwani.  Mtangazaji wa Clouds Fm Adamu Mchomvu, akiyaendeleza mastori ndani ya kitaa cha Taili tatu eneo la Magaoni, Kata ya Mabawa, Tanga.  Mwanadada Loveness Love akiwa na Gossip Cop Tz, Sudi Brown. Vijana walijitahidi kuonyesha umahili wao wa kuchana michano.    Clouds Tv nayo haikukosa.   Mazungumzo ya mtaani yakiendelea.   Mtangazaji wa Clouds Fm Adamu Mchomvu na Mwanadada Loveness Love.  Hapa jamaa alikuwa akitiririka machache ndani ya Clouds Fm/Clouds TV.  Producer wa Home record ya Tanga nae akimwaga maneno yake juu ya tamasha  fiesta. ...

REDDS MISS MWANZA 2012

Image

HABARI LEO

Image

PICHA NYINGINE ZA TIMU YA YANGA IKIWA RWANDA

Image
Yanga ambao wako Rwanda kuweka kambi na kutii mwaliko wa Rais Paul Kagame pia, hapa ni walipokua wamekwenda kutembelea nyumba ya makumbusho ya waliouwawa katika mauaji ya kimbari mwaka 1994. . . . Hapa ni kwenye uwanja wa mazoezi nyuma ya Amahoro.

MAGAZETI YA LEO AUG 23 NA STORI ZAKE KUBWA ZA HARDNEWS NA MICHEZO

Image
. . . .

Airtel Rising Stars Tanzania yatoka sare na Burkina Fasso

Image
Michuano ya Afrika Airtel Rising Stars Tanzania yatoka sare na Burkina Fasso Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Airtel Rising Stars kwa nchi za Afrika, (leo hii)  imetoka sare ya bao 1-1 na Burkina Fasso,katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Nyayo, jijini Nairobi. Matokeo hayo yanaiweka Tanzania shakani kusonga mbele katika michuano hiyo baada ya jana kuianza vibaya kwa kukubali kufungwa bao 1-0 na Gabon katika mchezo wake wa kwanza. Kufuatia matokeo hayo Tanzania inasubiri bahati tu ili kusonga mbele kwani sasa itabidi kushinda mchezo wake wa mwisho utakaofanyika kesho 23/08/2012 dhidi ya Zambia na wakati huo huo kuiombea Gabon iifungwe na Zambia katika mchezo wao wa mwisho.  Kila kundi itatoa timu moja kusonga mbele hatua ya robo fainali zinazotarajiwa kuanza kesho kutwa. Katika mchezo wa jana, Burkina Fasso ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata   bao la kushtukiza katika dakika ya kwanza ya kipindi cha pili na hivyo kuwafanya v...

Kiongozi Mstaafu wa Freemasons Afrika Mashariki,Sir Andy Chande atinga clouds Media Group

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga akizungumza na Kiongozi Mstaafu wa Freemasons Afrika Mashariki,Sir Andy Chande ofisini kwake mapema leo mjengoni hapo,ambapo baadaye pia alifanya ziara fupi na kujionea vitengo mbalimbali vya kampuni hiyo namna ambavyo vinafanya kazi. Mazungumzo yakiendelea ya hapa na pale. Kiongozi Mstaafu wa Freemasons Afrika Mashariki,Sir Andy Chande akisikiliza jambo kwa umakini. Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akiagana na wageni wake mara baada ya kufanya mazungumzo nao mapema leo,kwenye ofisi za kampuni hiyo,Mikocheni jijini Dar. Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akiagana na mgeni wake Kiongozi Mstaafu wa Freemasons Afrika Mashariki,Sir Andy Chande. Kiongozi Mstaafu wa Freemasons Afrika Mashariki,Sir Andy Chande akiondoka taratiibu mjengoni Clouds Media Group mapema leo mara baada ya kufanya ziara fupi kwenye ofisi hizo na kujionea mambo lukuki yana...