WAZIRI MKUU MSTAAFU AWASHAURI WABUNGE KUANZISHA SHULE
Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa (wa pili kushoto) akijumuika pamoja na Baadhi ya Wabunge wanaounda timu ya Bunge Sports inayoundwa na wabunge kutoka Baraza la Wawakilishi na Bunge la Jamhuri, wakati wa Chakula cha Mchana alichowaandalia Nyumbani kwake, Ngarashi Wilayani Monduli. Wengine pichani kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo,Amos Makalla, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Iddi Azzan pamoja na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Monduli, Reuben ole Kunai. WAZIRI Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa amewashauri wabunge wa timu ya Bunge Sports kufikiri juu ya kutunga sera ya michezo itakayoruhusu kuanzishwa kwa Shule za Michezo (Sports Academy) hapa nchini. Lowassa ameyasema hayo jana, baada ya kuialika nyumbani kwake timu hiyo iliyopiga kambi ya jijini Arusha tayari kwa mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki jijini Nairobi. “Nilisikitika kweli Timu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars il...