MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA
WAFANYABIASHARA watano, Said Bakhressa Gulam Dewji, Rostam Aziz,
Reginald Mengi na Ali Mufuruki, wametajwa na Jarida la Ventures Africa
linalozungumzia masuala mbalimbali ya uchumi wa Afrika kuwa ndiyo
matajiri zaidi nchini.
Anayeongoza katika orodha hiyo ni Bakhressa anayemiliki mali na fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 620 milioni sawa na Sh992 bilioni (Dola moja Sh1,600) akifuatiwa na Dewji ambaye utajiri wake ni Dola 560 milioni (Sh896 bilioni). Wengine na kiasi cha mali na fedha wanazomiliki kwenye mabano ni Rostam (Sh672 bilioni- Dola 420 milioni) Mengi (Sh448bilioni- Dola 280 milioni) na Mufuruki (Sh176 bilioni - Dola 110 milioni)-source Mwananchi magazine.