Posts

Showing posts from July 3, 2012

TUME YAANZA KAZI YA KUKUSANYA MAONI YA KATIBA SIKU YA JANA TAREHE 2 JULAI 2012

Image
 Mwananchi wa Kijiji cha Mtende Makunduchi Aziza Mcha, akikabidhi barua yake yenye maoni yake kwa Mwenyekiti wa Mkutano wa kutowa maoni ya mabadiliko ya Katiba ya Tanzania Mohammed Yussuf Mshamba, wakati tume hiyo ilipofika katika Wilaya ya Kusini Unguja kukusanya maoni ya Wananchi kuhusu Katiba, mkutano huo umefanyika katika viwanja vya Skuli ya Mtende.  Mwananchi wa Kijiji cha Mzuri Makunduchi Duli Ali Duli, akichangia maoni yake kwa Tume iliofika kukusanya maoni ya Wananchi kuhusu Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania, amesema kuwe na Serikali mbili ya Zanzibar na Tanganyika, na kuondoa kasoro zilioko katika Muungano huu. Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Balozi Salim Ahmed Salim, akizungumza kuhusiana na utoaji wa maoni ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya Mtende.

VODACOM NDANI YA SABA SABA

Image
 Mteja aliejitokeza katika maonesho ya sabasaba akipata maelezo ya namna ya kutumia simu ya ZTE 502 pia iliyokuwa na muda wa maongezi wa shilingi elf 6000 na kuuzwa kwa shilingi elfu 13 ikiwa ni ofa maalum katika maonesho hayo ya sabasaba. Wakala wa Vodacom M PESA akitoa huduma ya M- PESA kwa mteja alietembelea maonesho ya sabasaba jijini Dar es. Kampuni ya Vodacom Inashiriki katika maonesho hayo kama mdhamini rasmi wa mawasiliano.

BWA. VICENT LYIMO WA KIBOSHO AKABIDHIWA ZAWADI YAKE YA PIKIPIKI KUTOKA SERENGETI

Image
Meneja wa bia ya Serengeti Bw. Allan Chojo kushoto akiongea na waandishi wa habari na wakazi wa kibosho mkoani Kilimanjaro wakati wa kukabidhi zawadi ya pikipiki mpya kwa mshindi wa zawadi hiyo Bw Vicent Lyimo kulia, aliyejishindia kupitia promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na  inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti (SBL). Katikati ni mke wa Bw Vicent Lyimo Bi. Jesca Vicent Lymo. Picha 02 huku  Bw. Vicent Lyimo na mkewe  wakiwa juu ya pikipiki yao baada ya kukabidhiwa na Bw.Allan Chonjo

WATEJA WA AIRTEL SABASABA WAENDELEA KUJIZOLEA ZAWADI VIWANJA VYA SABA SABA

Image
Airtel ilivyojipanga na zawadi kwaajili ya wateja wake wanaonunua bidhaa mbali mbali na kulipia kwa njia ya Airtel money. ukinunua bidhaa katikakijiji cha Airtel, banda la Windhoek, hupata kuponi ambazo baadae huzungushwa na huibuka washindi wa kati ya zawadi hizo zikiwemo simu za mkononi aina ya sumsung, Modem yenye kasi ya 3.75G pamoja na shilingi 2,000 kwa jumla ya wateja 60 kwa siku Katika picha juu niKushoto ni meneja uhusiano wa Airtel Tanzania akifuatilia watoa huduma wa banda la Windhoek wanavyoelekezena jinsi ya kununua bidhaa katika banda lao kwa kutumia huduma ya Airtel Money Hizi ni bidhaa za Airtel na Windhoek ambazo ni zawadi za washindi  zikiwa zimepangwa maalum kwa ajili ya wateja kujishindia MC na mtangazaji wa ofa katika banda la Windhoek akitangaza namba ya mshindi wa simu katika kuponi wakati wa Bahati nasibu ya Airtel ilipochezeshwa  jana maalum kwa wateja wake wanaonunua bidhaa mbalimbali katika maonyesho ya 36 ya biashara kwenye viwa...

TEMEKE YAICHAPA DODOMA 2-0 COPA COCA COLA

Image
Temeke imefainikiwa kuilaza Dodoma mabao 2-0 katika mechi ya kundi C ya michuano ya Copa Coca-Cola iliyochezwa leo (Julai 3 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe, Dar es Salaam.   Mabao ya washindi ambao kwa matokeo hayo sasa wamefikisha pointi tano yalifungwa dakika ya tano Hassan Kabunda wakati la pili lilifungwa dakika ya 34 na Abdul Hassan.   Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam umeshuhudia Morogoro ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Iringa lililofungwa dakika ya 37 na Mutalemwa Katunzi.   Nayo Kilimanjaro imeibuka na ushindi wa bao 1- dhidi ya Tabora katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani. Bao hilo katika mechi hiyo ya kundi D lilifungwa dakika ya 14 na Eric Christopher.   Kwa matokeo hayo Tabora imebaki na pointi tatu baada ya kushinda mechi moja tu dhidi ya Pwani, na imebakiza mechi moja dhidi ya Kusini Unguja ambayo hata ikishinda haiwezi kuingia hatua ya 16 bora.   Nao mabi...

FAN SIMBA CLUB KUTOA ZAWADI

Image
Afisa habari wa mabingwa wa soka wa Tanzania, Simba SC, Ezekiel Kamwaga (kulia) akimkabidhi  ufunguo mpenzi wa timu hiyo  Abubakari Hamis (katikati) kutoka Arusha baada ya kuibuka mshindi katika bahati nafasi ya Simba Fan Club katika hafla fupi  jana. Kushoto ni meneja wa kampeni hiyo, Talib Rashid kutoka kampuni ya Push Media Moobile. Washiriki wa bahati nasibu hiyo wanatakiwa kutuma neno Simba kwenda kwenye namba “15678” na kuingia katika droo. KLABU ya Simba imewataka wapenzi na mashabiki wake kuendelea kujiunga na huduma ya kutuma ujumbe mfupi kupitia huduma ya Fan Simba Club ili kupata taarifa mbalimbali za Simba ikiwemo matokeo ya michuano ya kombe la Kagame  inayoanza Julai 14 mwaka huu na masuala ya Usajili. Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Klabu hiyo Ezekiel Kamwaga alisema kupitia huduma hiyo mashabiki wa Simba watapokea taarifa  za kila siku  ambazo wao watakuwa wa kwanza kuzipata kupitia huduma hiyo. Alisema pia itaisaidi...
Image
Warembo wanaotarajia kupanda jukwaani kuwania Taji la Miss Vyuo Vikuu 2012, siku ya Ijumaa wiki hii katika Ukumbi wa Maisha Club, wakipozi kwa picha ya pamoja nje ya Ukumbi wa Bunge, wakati warembo hao walipofika kutembelea na kujifunza shughuli za Bunge mjini Dodoma Leo, Julai 03, 2012.  Warembo wanaotarajia kupanda jukwaani kuwania Taji la Miss Vyuo Vikuu 2012, siku ya Ijumaa wiki hii katika Ukumbi wa Maisha Club, wakipozi kwa picha ya pamoja nje ya Ukumbi wa Bunge, wakati warembo hao walipofika kutembelea na kujifunza shughuli za Bunge mjini Dodoma Leo, Julai 03, 2012
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII INAWATANGAZIA MADAKTARI WOTE WANAOFANYA MAFUNZO KWA  VITENDO ( INTERNS),  WALIOPEWA BARUA ZA KURUDIS HWA  KWA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII , WANATAKIWA KURIPOTI MAKAO MAKUU YA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII  IFIKAPO SIKU YA IJUMAA  TAREHE 6 JULAI, 2012. IMETOLEWA NA: KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI 3/07/2012
Image
Mwenyekiti Barclays ajiuzulu Marcus Agius Marcus Agius aliamua binafsi kujiuzulu kutokana kwa kile alichotaja katika taarifa yake ya kujiuzulu kama pigo kubwa linalotokana na kuharibiwa sifa kwa kampuni hiyo kwa sababu ya madai ya kuwalaghai wateja kupitia nyongeza haramu ya riba. Wito umetolewa kuwa afisa mkuu mwandamizi wa kampuni hiyo, Bob Diamond ajiuzulu, kwa sababu alikuwa akisimamia uwekezaji wa benki hiyo wakati mpango ulipofanywa kulaghai wateja kupitia kwa riba inayotozwa katika benki hiyo. Hata hivyo wakurugenzi wa Barclays wameamua kuwa Bwana Diamond ataendelea kufanya kazi. Kwa hivyo Bwana Agius, ambaye pia ni mwanachama wa Bodi, aliamua, huku akiungwa mkono na wenzake, kujitwika lawama zote zinazotokana na madhambi yanayokabili Benki ya Barclays na hasira yote waliyo nayo wenye hisa wa benki hiyo. Mtu anayetazamiwa kuchukua mahali pake ni mkurugenzi mwingine, Sir Mike Rake, ambaye kwa sasa atalazimika kujiuzulu vyeo vyake vya kuwa mwenyekiti wa Ea...
Image
Timbuktu tomb attack is an attack on our humanity Islamist militants destroying the ancient shrine of a Muslim saint in Timbuktu, Mali, on July 1, 2012. This attack is led by a tiny armed minority, who violently imposes its interpretation of a faith on a distraught local community, spoiling centuries of tolerance and exchange. The Old Mostar Bridge, the giant Buddhas of Bamiyan, and now the Mausoleums of Timbuktu. Once again, culture is under attack. Militants from the Ansar Dine group, which controls much of northern Mali, have started to destroy Timbuktu's ancient tombs. In three days, half of the town's shrines have been destroyed in a display of fanaticism. In rebel hands since January, Timbuktu has been taken beyond the pale. Mali has gone from one of West Africa's most stable democracies to a country gripped by chaos, where over 300,000 people have been uprooted. The destruction of Timbuktu's shrines  adds a moral and cultural crisis to a...
Image
Syria yadaiwa kukiuka haki za kibinadam Shirika la Human rights watch Shirika la kutetea haki za kibinadam la Human Rights watch, ambalo limechapisha ripoti kuhusu kile kilichotaja kama sera ya serikali ya Syria, ambayo ni sawa na uhalifu na ukatili dhidi ya binadam. Ripoti hiyo imenakaili mahala ambako serikali ya nchi hiyo imejenga vituo vya kuwazuia wapinzani wake na mbinu ya mateso inayotumika. Shirika hilo limetoa wito kwa wale wanaohusika kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya Kimataifa ya jinai ICC. Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Haque, amesema viwango vya vitendo vya kikatili vinavyotekelezwa na serikali ya Syria Dhidi ya raia wake ni vya kushangaza. Amesema wahusika wote wanapaswa kuwajibishwa. Awali afisa mkuu wa umoja wa mataifa anayehusika na haki za kibinadam Navi Pillay ameonya kuwa viwango vya ukiukwaji wa haki za kibinadam vinaendelea kuongezeka nchini Syria. Pillay, amesema ghasia nchini Syria, zinaendelea kuchochewa na ku...