MISS KIGAMBONI YATOA MSAADA
SEHEMU ya mapato yatakayopatikana katika shindano la urembo la kitongoji cha Kigamboni mwaka huu yataenda kusaidia ukarabati wa madarasa yaliyopo kwenye Shule ya Msingi Kigamboni iliyopo jijini Dar es Salaam imeelezwa. Shindano la urembo la kitongoji cha Kigamboni linatarajiwa kufanyika Juni 15 kwenye Ukumbi wa Navy Beach kuanzia saa 1:00 usiku. Akizungumza jana, Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu, alisema kuwa wameamua kutoa sehemu ya fedha zitakazopatikana kwa lengo la kuipa heshima ya shule hiyo ambayo ni moja ya sehemu zilizotoa washiriki wa kinyang'anyiro hicho na wajumbe wa kamati ya maandalizi. Alisema kuwa wanawaomba wakazi wa Kigamboni na wengine kutoka sehemu mbalimbali jijini kujitokeza kushuhudia warembo wao ambao hapo baadaye wataenda kukiwakilisha kitongoji hicho kwenye mashindano ya Kanda ya Temeke. Aliongeza kuwa katika kusindikiza shindano hilo, bendi muziki wa dansi ya FM maarufu kama 'Wazee wa Ngwasuma' pamoja na msanii wa vic...