RAGE AWAKA

Rage amesema leo mchana katika Mkutano na Waandishi wa
Habari, makao makuu ya Simba, Mtaa wa Msimbazi kwamba ushahidi wa Yanga
kumsajili Yondan wakati amekwishasaini Simba, ni picha anayoonekana akisaini
wakati amevaa jezi mpya ya timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars yenye
nembo ya wadhamini wapya, Kilimanjaro Beer.
Rage amesema kwamba kitendo walichofanya Yanga ni uhuni ni
kinautia aibu mchezo wa soka, hivyo amewaagiza mawakili wa klabu hiyo kukaa leo
kuandaa mashitaka ya kupeleka FIFA.
Aidha, Rage alionyesha nakala ya mkataba ambao Simba
imesaini na Yondan, ikionyesha amepeaa fedha taslimu Sh. Milioni 25 kwa miaka
miwili.
“Simba Sports Club imesikitishwa na kitendo cha Young
Africans kuvunja taratibu za usajili kwa kumrubuni mchezaji wake Kelvin Patrick
Yondan, kwanza kwa kuzungumza naye na baadaye kwa ushahidi wa picha kuonekana
wakimuandikisha makaratasi ambayo baadaye imeripotiwa na vyombo vya Habari
kwamba alikuwa akisaini mkataba wa kuichezea timu hiyo ya Young Africans,” alisema
Rage.
![]() |
Nakala za mkataba wa Yondan na Simba SC |
Alisema Yondan ni mchezaji halali wa Simba SC aliye na mkataba hadi Mei 31, mwaka 2014, baada ya kuongeza mkataba na klabu yake, Desemba 23, mwaka jana. Mkataba wa awali wa Yondan Simba uliisha Mei 31, mwaka huu. “Sheria za FIFA za hadhi na uhamisho wa wachezaji ziko wazi, katika kipengele cha 5 kifungu kidogo cha 2 kinasema kwamba mchezaji atasajiliwa kuichezea timu moja tu kwa wakati mmoja,”alisema Rage.
Mapema jana BIN ZUBEIRY 'ilifichua' Yondan kusaini Yanga kwa Sh. Milioni 30, mkataba wa miaka miwili- maana yake mchezaji huyo amekunja zaidi ya Sh. Milioni 55 kwa mikataba yote.
Lakini Yondan mwenyewe jana aliukana mkataba wa Simba, akisema hajasaini.