Posts

Showing posts from October 26, 2012

Rais Kikwete alishiriki Swala ya IDDI kijijini Msoga leo

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika swala ya Iddi katika Masjid Rajab kijijini kwake Msoga-Chalinze leo Asubuhi. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono wa Iddi na baadhi ya waumini walishiriki swala ya Iddi katika Masjid Rajab Kijijini kwake Msoga, kata ya Chalinze,Wilayani Bagamoyo leo asubuh

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI MSIKITI MPYA WA JIHAD WILAYA YA MWANGA-KILIMANJARO

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika Jengo  la Msikiti mpya wa Jihad, baada ya kuzindua rasmi Msikiti huo uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa  Kilimanjaro, leo Oktoba 26, 2012 wakati wa Sikukuu ya Eid El Hajj, iliyofanyika sambamba na uzinduzi wa Mfuko wa  uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre. Picha na  OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini wa Dini ya  Kiislam katika Swala ya Idd El Hajj, iliyofanyika Kitaifa katika Msikiti mpya wa Jihad, uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya  Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro. Ibada hiyo ilifanyika sambamba na uzinduzi wa Msikiti huo na uwekaji wa Jiwe la Msingi. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakat...

POLISI WAWATAJA WAUAJI WA KAMANDA BARO

Image
 Pichani kulia ni  Mkurugenzi wa makosa ya Jinai Nchini (DCI) Robert Manumbaa akiyataja majina ya watuhumiwa hao wa mauaji ya Kamanda Barlo,na shoto ni IGP Said Mwema. JESHI la Polisi limewataja watuhumiwa 10, na bado linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine, ambao inadai walishiriki kumuua aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow. Kati ya watu hao watano wametiwa mbaroni Mwanza  na watu watano kutoka Dar es Salaam.  Leo (jana) mjini Mwanza, mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Said Mwema, Mkurugenzi wa makosa ya Jinai Nchini (DCI) Robert Manumba aliwataja watuhumiwa  hao ni Muganizi Michael Peter (36) mkazi wa Isamilo ambaye inadaiwa alikiri mwenyewe kumuua kamanda kwa risasi. Wengine ni Chacha Waitara Mwita (50), Magige Mwita Marwa, Bugazi Edward Kusota na Bhoke Mara Mwita (42) ambao walikamatwa jijini Dar es Salaam baada ya kuwekewa mtego kwa msaada wa wananchi. Wanaoshikiliwa...

WARUDISHWA RUMANDE

Image
VIONGOZI WA UAMSHO WARUDISHWA TENA RUMANDE by John Bukuku on October 25, 2012 in JAMII with No comments Baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Sheikh Farid Hadi Ahmed kushoto akiwa na wenzake sita walioletwa Mahakama kuu Zanzibar Vuga wakiwa hawana ndevu na kufunguliwa mashtaka manne mapya mahakamani hapo yakiwemo kuharibu mali za watu zenye thamani ya Shl.Milioni 50 na kufanya vurugu za makusudi zakuhatarisha amani katika nchi…Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar Baadhi ya Askari wa kutuliza fujo wakiwa Mahakama kuu Zanzibar Vuga kwa lengo la kutuliza amani Mahakamani hapo.. Picha na MakameMshenga-Maelezo Zanzibar Baadhi ya Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO wakiwa wanatoka katika Mahakama Kuu ya Zanzibar Vuga baada ya kufunguliwa mashtaka manne mapya..Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar Mawakili wa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Abdallah Juma kushoto na Salim Tawfik wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu kujitoa kwao sik...

COOMING SOON........

Image

RAIS WA ZANZIBAR ASHIRIKI SALA YA EID EL HAJJ

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein,pamoja na Viongozi wengine wakijumuika na waislamu na wananchi katika  swala ya EID el Hajj katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar Leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] Baadhi ya Waislamu na wananchi wakisikiliza Hotuba,baada ya Swala ya Eid el Hajj iliyotolewa na Sheikh Soraga,katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar Leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na waumini ya Dini ya Kiislamu baada ya kuswali swala ya  EID el Hajj katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar Leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]