POLISI WAWATAJA WAUAJI WA KAMANDA BARO
Pichani kulia ni Mkurugenzi
wa makosa ya Jinai Nchini (DCI) Robert Manumbaa akiyataja majina ya
watuhumiwa hao wa mauaji ya Kamanda Barlo,na shoto ni IGP Said Mwema.
JESHI
la Polisi limewataja watuhumiwa 10, na bado linaendelea kuwatafuta
watuhumiwa wengine, ambao inadai walishiriki kumuua aliyekuwa Kamanda wa
polisi mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow.
Kati ya watu hao watano wametiwa mbaroni Mwanza na watu watano kutoka Dar es Salaam. Leo
(jana) mjini Mwanza, mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania
IGP Said Mwema, Mkurugenzi wa makosa ya Jinai Nchini (DCI) Robert
Manumba aliwataja watuhumiwa hao ni Muganizi Michael Peter (36) mkazi
wa Isamilo ambaye inadaiwa alikiri mwenyewe kumuua kamanda kwa risasi.
Wengine ni Chacha Waitara Mwita (50),
Magige Mwita Marwa, Bugazi Edward Kusota na Bhoke Mara Mwita (42) ambao
walikamatwa jijini Dar es Salaam baada ya kuwekewa mtego kwa msaada wa
wananchi.
Wanaoshikiliwa jijini Mwanza kwa
mahojiano ni pamoja na Mwalimu Doroth Moses Lyimo aliyekuwa na RPC
wakati mauaji yakitokea, Felix Felician Minde (50), Philemon Felician
(46) maarufu kama Fumo, Bahati Agustino Lazaro (28) na Amos Magoto (30) maarufu kama Bonge.
Manumba amesema simu iliyoporwa ya
mwanamama ambaye alikuwa akisindikizwa nyumbani na marehemu, ndiyo
imesaidia kukamilisha upelelezi huo na hatimaye wahusika kukamatwa.
Alisema Kikosi kazi cha upelelezi
kilichokuwa chini yake Manumba kilijigawa kwenye makundi matatu moja ni
lile la Ukamataji, Mahojiano na lingine la interejensia huku wakitumia
njia ya sanyansi kwa kufuatia mitandao ya simu.
Marehemu Kamanda Barlow aliuawa usiku
wa Oktoba 12 majira ya kati ya saa 7 na 8 usiku katika eneo la Mianzi
Mitatu, Kitangiri, kona ya Bwiru baada ya kupigwa risasi na watu
wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wakati alipopita kumsindikiza Mwalimu
Dorothy Moses nyumbani kwake kutoka katika kikao cha harusi
kilichofanyika Mtaa wa Rufiji.