Posts
Showing posts from September 29, 2012
ZITTO AUTAKA URAIS 2015
- Get link
- X
- Other Apps

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2015 badala yake anajipanga kuwania urais. Zitto alisema hayo jana alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliokuwa unafanyika maeneo ya Soko la Mwanga, mjini Kigoma. Zaidi ya watu 200, ambao walihudhuria katika mjadala huo wa wazi walimuuliza maswali mbalimbali mbunge huyo, huku mmoja akigusia kuhusu tetesi za mara kwamba Zitto anataka kugombea urais katika uchaguzi ujao. “Nimefanya kazi kubwa katika kazi yangu ya ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka kumi. “Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na s...
MAONYESHO YA SARAKASI YA MAMA AFRIKA YAENDELEA KUWA YA MFANO HUKO NEW WORLD CINEMA DAR.
- Get link
- X
- Other Apps
"Karibuni watanzania wote muone sarakasi na utamaduni wa kitanzania". Trade Marketing Supervisor wa kampuni ya simu za mkononi ya TIGO ambao ndio wadhamini wakuu wa maonyesho ya 'Sarakasi ya Mama Afrika' yanayoendelea katika viwanja vya New World Cinema Bw. Gaudens Mushi akiwakaribisha wageni waliohudhudhuria onyesho hilo. kushoto ni Afisa Mahusiano wa TIGO. Pichani Juu na Chini ni mfululizo wa maonyesho ya sarakasi ya 'Mama Africa Circus'. Picha Juu na Chini ni baadhi ya wadau walioshiriki maonyesho hayo wakifurahia. Posted in:
Rais Kikwete awaaga mabalozi wa Iran na Cuba
- Get link
- X
- Other Apps

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Cuba nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Mhe Ernesto Gomes Dias leo Septemba 28, 2012 Ikulu jijini DAr es salaam Dar es salaam. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Iran nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Mhe Mohsen Movahhedi Ghomi leo Septemba 28, 2012 Ikulu Dar es salaam