ZIARA YA MKUU WA MKOA WA RUKWA
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongea kwa ukali wakati akionyeshwa ramani na Mpima wa Manispaa Selice Nzyungu ya eneo alilouziwa muwekezaji Ephatta Ministry na lile walilopewa wananchi wa kata ya Mollo katika Manispaa ya Sumbawanga. Mkuu huyo wa Mkoa amelazimika kutembelea eneo hilo baada ya kupewa taarifa za awali na Kamati aliyoiunda katika kufuatilia mgogoro unaoendelea kati ya muwekezaji na wananchi wanaolizunguka shamba hilo. Lengo kuu la ziara yake hiyo ya tarehe 02, Septemba 2012 ilikuwa ni kutembelea mashamba yakiwemo ya muwekezaji na wananchi pamoja na kuzungumza na wananchi na muwekezaji kwa kuchukua kero zao kwa ajili ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo. Mkuu huyo wa Mkoa wa Rukwa akizungumza kwenye Mkutano na wananchi wa kata ya Molo ambapo pia wawakilishi wa muwekezaji walialikwa kuskiliza na kutoa kero zao mbele ya wananchi wa kata hiyo. Hata hivyo baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kusikiliza kero hizo aliwaahidi wananchi pamoja n...